Zamani Ikulu ilipelekewa orodha ya graduate wote, siku hizi inapelekewa orodha ya Viongozi wa CCM ngazi ya kata hadi Taifa

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
5,222
2,000
Habari!

Siku moja nilikuwa na mzee mmoja mstaafu JWTZ aliniambia kuwa Ikulu hupokea taarifa na majina ya wahitimu wa elimu ya chuo kikuu wale wa degree ya awali nakuendelea. Pia hupokea majina ya baadhi ya wahitimu wa elimu ya stashahada na advanced diploma kila mwaka.

Rais kwa kutumia team yake huwafanyia vetting kwa ajili ya teuzi. Lakini sasa inaonyesha ni dhahiri Ikulu inapokea majina ya makada wa CCM tu ili kuyaweka kwenye kanzi data kwaajili ya teuzi mbalimbali.

Makazini humu kuna watumishi wana digrii moja mpaka 3 wengi tu, wamekaa kwenye utumishi wa umma miaka zaidi ya 20, teuzi zikitoka kila nikichungulia siwaoni.

Kwa mtindo huu tutafika kweli kwenye uchumi halisi wa kati
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,946
2,000
Me saiz nawaza kuchukua kadi ya ili niungane nao huko huko, if u can't fight them join them.
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,096
2,000
Umenitekenya! Kuna mwanamke (darasa la saba, hata kuandika ni shida) alipewa nafasi ya mwenyekiti wa wanawake ngazi ya wilaya . Kumbuka wasomi wanawake ni wengi katika hivyo wilaya, tutafika??.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom