Zamani DCI na DPP walikuwa chini ya IGP na ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa unanyooka tofauti kabisa na baada ya maboresho!

Huwa sielewi ni kwanini mashahidi wa mashtaka huwa wanapata wakati mgumu wanapohojiwa na mawakili wa utetezi na hasa ikizingatiwa kuwa mashahidi wa Jamhuri huandaliwa na DPP tena mashahidi wengine ni wanasheria kitaaluma ( wana LLB )!!

cc: Pascal Mayalla
Ni kwa sababu hawakuandaliwa mapema, kwa kukumbushwa ni nini walichokisema awali na wanatakiwa waeleze itu gani, kwa kiwango gani na majibu yaweje wanapohojiwa na mawakili na wanasheria wabobezi wa kesi mahakamani.

Wachunguzi kutojiendeleza zaidi kwenye taaluma ya sheria, uchunguzi, na utaalamu wa fani mbali mbali hadi kufika kiwango cha shahada za uzamili na uzamivu kupitia mazoezi ya kutosha yenye changamoto zilizopatiwa ufumbuzi wa kisayansi.

Wanatakiwa wasome kwa kiwango cha kutukuka masomo ya MSc/PhD in crimes, investigations and intelligence ndio wanaweza kuendana na mawakili wanaofanyakazi za kimahakama kila siku bila hivyo wataendelea kudhalilishwa kwa kuwa na maelezo yanayokinzana kila mara.
 
Back
Top Bottom