Ndugu wanajamii naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hili tunda. Kwa ufahamu wangu siku zote nilifahamu Zeituni ni "Olives", na olives nafahamu ni matunda madogo saizi ya white grapes na mara nyingi huwa naona sura yake inakaribia kufanana na white grapes. Sasa tatizo ni kwamba ktk kipindi cha Dr. Ndodi kinachorushwa EATV alikuja na tunda fulani kubwa la njano lenye umbo la yai akasema ndio zeituni. Sasa nilitaka kujua kuna zeituni nyingine zaidi ya Olive? Na pia lile tunda alilokuja nalo akasema huwa yanapatikana Mbeya na yanaitwa mazeituni kwa Kiingereza linaitwaje?