Zain yadhamini wanafunzi wanane

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
ZAIN, kampuni ya simu za mkononi yenye mtandao katikanchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imetangazamajina ya wanafunzi wanane watakaosomeshwa bure nakampuni hiyo kupitia mradi wa Build Our Nation (BON)wa Zain.

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, TunuKavishe alisema Dar es Salaam jana kuwa huo nimwendelezo wa ofa ambayo hutolewa na Zain kila mwakaya kuwasomesha wanafunzi wanane bora wa kike na kiumewa Tanzania wanaopata ruhusa kutoka vyuo vikuu nchini.

Alisema wanafunzi hao wanane waliochaguliwa ambao katiyao wanne ni wavulana na wanne ni wasichana, ni walewaliofaulu vizuri zaidi katika mitihani yao ya kidatocha sita, na wamechujwa kupitia Tume ya Vyuo VikuuTanzania (TCU).

Tunu aliwataja wanafunzi wavulana waliopata ofa yakusomeshwa bure mwaka huu na vyuo vikuu watakavyosomakatika mabano ni Michael Kihoko (Chuo Kikuu Mzumbe),Ernest Nsangalufu (Chuo Kikuu Dar es Salaam), RemmyMseya (Chuo Kikuu Dar es Salaam) na Nelson Mlay (ChuoKikuu Dar es Salaam).

Wasichana waliopata ofa ni Dorothea Kahindi (ChuoKikuu Dar es Salaam), Priscilla Mafuru (Chuo KikuuMzumbe), Queeny Kiwango (Chuo Kikuu Dar es Salaam) naSubira Exauty (Chuo Kikuu Dar es Salaam).

Alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2008,Zain itakuwa inasomesha wanafunzi 31 katika programuhiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 ambayo lengo lake nikuinua kiwango cha elimu nchini.

Katika Zain Scholarship, wanafunzi wanaopata ofawamekuwa wakilipiwa gharama zote na Zain kwa asilimia100 ikiwa ni pamoja na chakula na malazi, na piawamekuwa wakipewa ajira ya muda Zain wakati wa likizohuku wakilipwa.

Alisema sharti wanalopewa wanafunzi haowanaochaguliwa, ni kwamba wanatakiwa kuendelea kufauluvizuri katika mitihani yao ya vyuo vikuu. Tangu kuanzakwa mradi huo, tayari Zain imesomesha wanafunzi 23 namwaka huu wamehitimu watatu ambao ni Hawa Myamba(Mzumbe), Patrick Nobert (Chuo Kikuu cha Dar esSalaam) na George Peter (Mzumbe).

Kutokana na kuongezeka wanafunzi wanane wa mwaka huu,Zain itakuwa imesomesha jumla ya wanafunzi 31. Wenginewaliosomeshwa tayari ni Henry Kalisti (Chuo Kikuu chaDar es Salaam), Emmanuel Kassi (Chuo Kikuu cha Dar esSalaam), Judith Mtweve (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam),Omari Zuberi (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), RoseMillo (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Noel Mazoya(Chuo Kikuu cha Mzumbe). Venance William (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam),Athuman Ally (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), EdithTuruka (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Maureen Skauki(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Nyaura Kibinda (ChuoKikuu cha Dar es Salaam), Rukia Mwifunyi (Chuo Kikuucha Dar es Salaam), Baraka Andrew (Chuo Kikuu chaMzumbe), Boniface Chacha (Chuo Kikuu cha Dar esSalaam). Wengine ni Salome Maro (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam),Nathael Nelson (Chuo Kikuu cha Mzumbe), Mugeta Lufael(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Harold Madeha (ChuoKikuu cha Dar es Salaam), Jonia Kashalaba (Chuo Kikuucha Mzumbe) na Gemma Kamara (Chuo Kikuu cha Dar esSalaam).

Mbali na kusomesha wanafunzi, katika programu ya BONiliyoanzishwa Mei 10, 2004, Zain pia imekuwaikichangia vitabu kwenye shule za sekondari kwa mikoayote 26 ya Tanzania, na hadi kufikia mwishoni mwamwaka huu 2008, Zain itakuwa imetumia zaidi ya shmilioni 500 kutekeleza programu hiyo na zaidi ya shuleza sekondari 520 zitanufaika kutokana na mradi huo.
 
Back
Top Bottom