Zain, Wabunge na Ungo !!!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,791
22,224
wabunge.jpg
Mbunge wa Mbinga Magharibi,John Komba akicheza muziki wa African Stars 'Twanga Pepeta International' akiwa ameshika ungo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Zain Tanzania mjini Dodoma, wikiendi.

Haya Wana JF, je kwa mtindo huu tutegemee nini kwa watunga sheria wetu kama Waamuzi na Wachezaji wako timu moja ?

Celine_Bendera.JPG
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Joel Bendera akicheza na Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania,Celine Njuju,muziki ulioporomoshwa na African Stars 'Twanga Pepeta International'mjini Dodoma,wikiendi.

Na bado

Anna_Lupembe.JPG
Mbunge wa Viti Maalumu,Anna Lupembe(kushoto)akicheza muziki wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta International)na Mbunge wa Mbinga Magharibi,John Komba wakati wa hafla iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania mjini Dodoma,wikiendi


Duh, kazi kweli kweli !!!!

 
hicho anachofanya ndo proffessional yake,
uongozi kakutana nao tu on the way.
 
wabunge/ Viongozi nao ni watu jamani nao wanaruhusiwa ku-have fun. Ingawa ingekuwa vizuri wangekuwa wanafanya hivyo baada ya kufanya mambo mazuri na kuupinga ufisadi. ila sioni ubaya kwenye hizo picha.
 
Komba ananikumbusha yule mbunge alokutwa usiku wa manane kwenye mbuyu mkubwa pale namanga na ze comedy akihesabu matawi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom