Zain Tanzania Kubadilisha Jina na kuwa Airtel Jumatatu ijayo

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Baada ya kubadilisha jina kutoka Celtel kwenda Zain mwaka 2008, kampuni ya Zain inatarajiwa kuanza rasmi kutumia jina jingine jipya la Airtel kuanzia tarehe 22 November 2010 (jumatatu ijayo). Hii ni baada ya mmiliki wa Zain Afrika kuuza hisa zake kwa kampuni Airtel ya India.

Jina hilo litakalokuwa katika muonekano huu hapa chini, litakuwa na rangi nyekundu ambayo inafanana na rangi ya jina walilokuwa wanatumia hapo mwanzo la Celtel kabla hawajabadili na kuwa Zain.

thumb-airtel-logo.gif

Changamoto waliyonayo Airtel/Zain ni namna watakavyoweza ku manage perception ya wateja wao ambao asilimia kubwa hawana ujuzi wa masoko ya fedha na namna biashara za makampuni zinavyoendeshwa.

Karibu airtel, tunatarajia mapinduzi zaidi katika soko la mawasiliano. Binafsi ningependa makampuni ya simu yawekeze sana katika ubora wa mawasiliano. Kwa ilivyo sasa kampuni kama tiGo licha ya kuwa na bei nafuu lakini ubora wa network yao uko chini sana. With tiGo, drop calls ni nyingi sana mpaka zinaudhi!!
 
Ni kweli brooklyn but sio kama wanabadili jina kuepuka kodi coz najua kadri kampuni yakigeni inapotoa huduma flani nchini miaka ya mwanzo ulipa kodi ndogo kadri waendeleavyo kodi uongezeka,so uoni kama wanaepuka that kind of tax?Eg:buzz to tigo
 
hii ni furaha kubwa, kwasababu hapo itakuwa neutral kidogo,....jina la zain/zainabu lilikuwa halipendezi labda kwasababu lilitokea uarabuni...likiwa airtel nakwambia litavuna, na litabarikiwa.
 
MWEKEZAJI MPYA HUYO!kama makampuni ya mafuta,hotel yanavyobadilika,MBONA WANANCHI HATUAMBIWI SERIKALI KAMA MWANA HISA IMERIDHIA HUO MTINDO WA KUVUNA MWEKEZAJI NA KUONDOKA?ILE SHERIA YA KU LIST TEL COS KTK DSE VIPI?JK ATUJIBU
 
hii ni furaha kubwa, kwasababu hapo itakuwa neutral kidogo,....jina la zain/zainabu lilikuwa halipendezi labda kwasababu lilitokea uarabuni...likiwa airtel nakwambia litavuna, na litabarikiwa.

Inabidi na kiswahili tukibadilishe maana maneno mengi yanatokea huko mkuu.... can we insert someother words in swahili as well ili iende sambamba na kubadilisha jina zain kwenda airtel ifikapo 22/11/2010?
 
Mimi binafsi ni mteja wa hii kampuni toka zamani lakini sasa imenichosha. Celtel - Zain - Airtel - sijui nini? Hakuna kutulia?
 
huu ni ukwepaji kodi hakuna lolote.....tena hawa ni wahindi basi tumekwisha....serikali haipati kitu tena katika kodi...
ila airtel inafanya vizuri india na mwenye kampuni ana uwezo.
tindu lisu dr. Mwakyembe na wanasheria wenzenu .....tunaomba tusaidie katika hili la tax holidays kwa kampuni za kigeni libadilishwe
 
Hawa wanakimbia garama za kulipa kodi.

Kwa JINA jipya, UNA MAANISHA UMILIKI MPYA, na KAMPUNI MPYA...

Kwa kawaida mwekezaji anakuwa Exempted katika criteia ya mojawapo mamlaka ya mapato "exemption in CAPITA GOODS" ambayo kwa uhakika wa aasilimia 90 ni miaka mitano ya msamaha au zaidi..........

Ndo maana kwa kumbukumbu zangu haya majina/miliki haiwezi kuzidi miaka 6, NA ISITOSHE MATAJILI NI WALEWALE ila ni geresha ya kubadili jina la kimagumashi au mtu anapandikizwa ili waweze kupata hiyo exemption.

Hawalipi KODI kabisa zaidi ya "destination inspection fee" katika kila mizigo ya MABILIONI YA SHILINGI WAINGIZAYO TANZANIA KWA MIAKA 5.
Kumbuka Destination Inspection fee ni 1.2% ya gharama yoote ya mzigo.

Wakati huo anakuwa amekimbia KODI KIBAO kama VAT, Exice duty,Importation duties na nyinginezo ambazo kwa harakaharaka ni zaidi ya 50% ya gharama ya mzigo husika isipokuwa kwa malighafi.

So ikifika miaka mitano waliyopewa msamaha HUBADILI umiliki, maana wanapewa CERTIFICATE of INVESTOR mpya, kwa jina jipya LENYE MISAMAA MIPYA YA KODI KWA MIAKA MITANO MINGINE.

Ni kama kamchezo, ikiisha wanafanya tena MAANA ANAEULIZWA ANAPOOZWA...

Na kwa CELTEL-ZAIN-AIRTEL kuna madeni amabayo wanayakimbia katika utumiaji wa miundombinu ya TTCL, kwa kuwa gharama ni kubwa wanazodaiwa (sina uhakika kwa sasa ila wakati CELTEL-ZAIN deni lilifika 260bil nikosolewe kama sipo right). Tujiulize hizi pesa zimelipwa lkwa mfumo wa kuuziana ndeni (buy back) au NDO UFISADI MWINGINE HUU.

Tanzania pesa ipo,watu wanaweza kusoma bure chekechea -chuo kikuu, ila ni mifumo kama hii.

Pesa inayopotea kwa misamaa ya kodi for the next 5yrs kwa JINA JIPYA la AIR TEL ni nyingi mnoooooooo, alafu take it or leave it ITAUZWA TENA.

Na kikubwa apart from ukwepaji wa kodi MIMI kwa mtazamo wangu ni hilo deni la TTCL, maana CELTEL-ZAIN-AIRTEL ndo hawaishi kujibadilisha kwa kuwa baada ya miaka mitano wanabeba mzigo mkubwa saana wa kutakiwa kulipia, YAANI TAXES na malipo YA MIUNDOMBINU YA TTCL.

Kwa mtazamo wangu waangaliwe hawa watu wanaotoa vibalihivi, kwa sababu wanajua na ndio wanaoiba hizi pesa.

Tunaibiwa jamani.

Naionea huruma Tanzania yangu ya kesho.Ya mwanangu na mimi nikifika umri wa wazee wa EAC.
Duh
 
Hapa ndipo tunapohitaji watunga sera makini. Wakati bilionea Mo Abraham ananunua Celtel aliuziwa kwa bei cheee mnoo (nafikiri kulikuwa na kick back kubwa kwa Mkapa na wateule wake) lakini miaka 2 tu baada ya kuuzwa kwa Celtel na kuwa Zain Mo ameuza Zain ile ile ambayo haijawekeza chochote cha ziada ktk miundombinu kwa mabilioni ya dola kwa wahindi. Kweli inasikitisha sana kuona rasilimali zetu zinafaidisha watu wa nje na si sisi wazawa!
 
Mimi binafsi ni mteja wa hii kampuni toka zamani lakini sasa imenichosha. Celtel - Zain - Airtel - sijui nini? Hakuna kutulia?

Mimi binafsi what counts is value for money/if value propositions in terms of call/data charges,qualityof service etc are OK ,i really care less about name
 
Lakini mkuu huduma si ni zile zile tuu?
<br />
<br />
mkuu huduma inaweza kuwa tofauti dependin mwekezaji mpya anataka nini! Ngoja tuone wahindi watakuja na nini, Kifupi Zain walipoteza kwa kiasi kikubwa market share yao kwenda kwa tiGO na partly Vodacom.
 
Mambo yaanza kupamba moto Zain/airtel ndani ya Mlimani City Conference Hall!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom