Zain african challenge-donda la wanafunzi au wa-tz wote?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zain african challenge-donda la wanafunzi au wa-tz wote?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Apr 14, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Hata nami nimewahi kuwaponda kupitia thread moja hapa JF! Na wengi tu wamepata kuwaponda wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu jinsi wanavyuochemsha kujibu maswali wakati wa ZAIN AFRICAN CHALLEENGE! Hata hivyo, je miongoni mwenu yupo ambae ameshawahi kuchukuwa nafasi ya kuwa mmoja wa wananfunzi hao wakati maswali yanapoulizwa? Mara kwa mara nimekuwa nikijipa nafasi ya uanafunzi na kujaribu kujibu maswali yanayoulizwa pande zote mbili. Sio siri, mara nyingi nimekuwa nikiwapiga bao wanafunzi wetu- i mean mie nimekuwa nikijibu kwa usahii zaidi kuliko vile ambavyo wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu wanavyojibu. Hata hivyo, lazima niwe mkweli kwamba haijapata hata mara moja mimi kuwapiga bao wanafunzi wa vyuo vikuu vya nje! What i mean ni kwamba endapo nami ingetokea kuwa kwenye panel ya waulizwa maswali kwa upande wa vyuo vikuu vyetu, ningeweza kujibu vizuri angalau lakini nisingeweza kuwabwaga wanafunzi wa vyuo vya nje, hata hapo jirani KENYA!!! Huwa wakati mwingine hadi najiuliza vitoto hivi vimepata wapi majibu ya maswali ambayo katu sikuwa na idea nayo!! Yaani utazani jama wamekula DESA(SIMBI)!!!!!! Sasa swali kwako mdau; pamoja na kwamba tunawalaumu wanafunzi wetu, je endapo wewe ungekuwa pale mbele ungeweza kuwabwaga madent kutoka nje?! Kama huna jibu la swali hili, basi jumapili si mbali, jaribu kufuatilia na kujibu hayo maswali ukijilinganisha na madenti wa nje!! Wewe Si Dokta bana? Si una MASTERS mkuu? si una-hold LLB with Honor?! Hebu jaribu jumapili hii kujibu maswali sambamba na madenti wale?! Hofu yangu ni kwamba, huenda tatizo si wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu pekee, bali ni Watanzania kwa ujumla. Kama hutaki, basi ingia kwenmye panel jumapili hii na jumatatu utuletee jibu!!!!!!! Tunaishi kwa ujanja ujanja tu lakini maarifa hamna! Mfumo mbovu wa elimu na kutopenda kuchakura mambo ndiko kunakosababisha ubovu huu!! Si kwa wanafunzi tu, bali sote tuliopitia mfumo huu! Pamoja na li-PhD lako, au na u-Profesa wako, si ajabu wale madogo wa vyuo vikuu vya nje wnaweza kukuumbua kwenye ZAIN AFRICAN CHALLENGE. Kama tunabisha, tuwaombe ZAIN waandae shindano baina ya ma-graduate wetu VS madenti wa hapo jirani tu! Ukweli unauma, lakini ndio hali halisi!
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hahahaha niliona siku ile yule mwanafunzi wa Tumaini university akikodolea macho huku wenzie waki press kitufe na kujibu maswali kiulaini. Mfumo wetu wa elimu ni mbovu ajabu, sisi tunasomea mitihani tu na si kupata knowledge.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu kuna mdogo wangu alishawahi kushiriki.
  Ni kwamba, wiki chache kabla ya mpambano, washiriki wote mnapewa maswali yote yatakayoulizwa siku ya mpambano
  ila hamjui nyie mtaulizwa swali gani.
  so ni kazi ya washiriki kutafuta majibu ya maswali yote kabla ya mpambano ili ikitokea limemwangukia ajue atatoa jibu gani sahihi.
  Wenzetu wa Kenya na wengine inaonekana wanatafuta majibu ya maswali yote na ndio maana inakuwa simpo kutoa majibu tena kwa haraka.
  Kwa upande wa wanafunzi wa kwetu mmmh! nazani huwa hawayafanyii kazi yale maswali.
   
 4. C

  Cotan Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  "Makalio ya sufuria hayaogopi moto".kWANINI YAOGOPE MOTO WAKATI NDO KAZI YAKE!!!!!!!!!!!!!!!?????????????
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  LAkini kama kweli mnapewa maswali prior of the challenge then mnashindwa hilo ni pepo, si mnagawana maswali? waTZ tuna tatizo la kugawana majukumu katika utendaji wa kazi zetu ndio maana majuzi mkulu mmoja siku ya sherehe kapiga picha anagawa pipi kwa watoto. Yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani .................................. nisiseme mie, karibuni FURAHIDAY tuwavalie RED Tshirt :eek:
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Kutokana na maelezo yako sikushangaa ulipokiri mwenyewe kuwa 'ulipigwa bao'. Ona ulivyo na mawazo finyu.....
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  taratibu best huna haja sana ya kuingia kwenye ugonvi wa maneno. Ujue me naogopa ugomvi wowote kwa kuwa unakufanya usiwe na raha. Nakushauri best hata ukukasirika jitahiti kutokubali kufanya kama hasira yako inavyokuelekeza. Ni ushauri tu take it or leave it!
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,686
  Likes Received: 8,221
  Trophy Points: 280
  Kama ni elimu mkuu i stil apreciate our TZ education. Nilisoma my undergraduate degree in Kenya sam years back. I know what they learn especially in high school na zile common courses za university.
  Wabongo tunafundishwa wide na deep..ila kama ulivyosema kuna hulka ya kusomea pepa basi mambo yameisha!
  Halafu, hatuna hulka ya kusoma vitabu (widely and wildly)!
  Mi napenda hawa watu wanavyosoma..wanasoma various forms of literature! sasa wewe unadhani utafundishwa darasani Greek Mythology!??
  Let's go back to the reading culture!
  Mimi nilisoma hapo Africa Nazarene University-watch that space! those kids r going far..na i kan tel u hakuna kitu wanafundishwa darasani interms of the content of the questions..ni kumake better use of the Library and net!
  One love..Go Africa Nazarene University!!!!!!!
   
 9. bongo-live

  bongo-live JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2016
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 824
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 80
  atareee
   
 10. badiebey

  badiebey JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2016
  Joined: Nov 29, 2013
  Messages: 5,890
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Ohh this used to be one of my fav TV shows
   
Loading...