Hata hao UDSM,MHUMBILI,MZUMBE nk nao walikuwa na utumbo huohuo.Kwa hiyo hili ni tatizo la vyuo vyote.hakuna cha mwenye afadhali.Siyo kila taasisi hapa Tanzania inayojiita Chuo Kikuu ni Chuo Kikuu kweli. Baadhi kusema ukweli ni dignified high schools. Reading culture imepotea kabisa miongoni mwa wanafunzi. Hata magazeti hawasomi achilia mbali tamthilia na maandiko mengine yanayoelimisha. Sasa hiyo general knowledge wataipata wapi? They are a mirror reflection of what we have created.
Ndio maana nikasema tatizo ni foundation za wanafunzi. Huko walikotoka hawajapikwa vya kutosha. Kuna post humu kwamba professor wa Biology pale UDSM wanafundisha wanafunzi wao kiingereza,ujue hali ni mbaya mno!Hata hao UDSM,MHUMBILI,MZUMBE nk nao walikuwa na utumbo huohuo.Kwa hiyo hili ni tatizo la vyuo vyote.hakuna cha mwenye afadhali.
Wanifanya nilie kabisa mkuu..Zamani wakati tupo secondary tulikua na debating clubs. Wanaojitia wanajua kuharibu mitaala ya elimu wakafanya wanavyojua wao ikawa hakuna cha debate wala nini kwenye sec.schools. Sasa ukimwona huyo form six aliejoin chuo utajisikia huruma sana jinsi anavyoanza kusimama na kutoa hoja. Sijui tutaanzia wapi kurudisha tena uwezo wa wanafunzi wetu hapa bongo.
Wanifanya nilie kabisa mkuu..
Yaani nikikumbuka enzi hizo za debate clubs..sasa hivi nawauliza wadogo zangu wananiambia hakunaga kitu kama hicho!Inaudhi lakini...how do we even have members of parliament who can not present proposals and expect maendeleo??!
Nalia...pole!
Wapo busy na Mamushka!!We acha tu, enzi hizo ilikua mtu unadebate,unapingana na mtu kwa hoja,baada ya debate mpo marafiki na mnaenda mpirani bila shari wala kununiana. Ilikua inatufundisha mengi sana kupitia such things. Lakini siku hizi hao wanaoenda kututungia sheria wakitofautiana kwa hoja basi ni visasi mtupu!
Shida ya wanafunzi wa kiTanzania ni kuwa hawana "general knowledge".
Ukimwuliza mambo ya darasani anaweza akajaribu kidogo, tena isiwe kwa kuzungumza, labda aandike!!
Mfumo mzima wa elimu unahitaji kuangaliwa upya. Watoto hawapewi elimu kuhusu mambo ya nje ya darasa. Halafu na hii tabia sijui ni waziri yupi wa elimu aliingiza kuondoa tamthilia (literature) zisizokuwa za kiTanzania/ Afrika wakati dunia nzima inasoma Shakespeare mTanzania si ajabu anasikia jina "Shakespeare" kwa mara ya kwanza kwenye filamu!! Au Sherlock Holmes.
Najua kuna watakao sema ni ukoloni mambo leo, lakini sikubaliani na dhana hiyo, kujua kuhusu mila/ tamthilia za utamaduni tofauti na wa kwako kuna saidia sana kufungua macho na kupanua mawazo.
Bila mabadiliko vyuo vya Tanzania kwenye mashindano kama hayo unayozungumzia vitaendelea kuwa wasindikizaji tu