Zaidi ya watumiaji Billion 2 wa Google Chrome wapo hatarini data zao kukusanywa sana mitandaoni

Chrome wkt mwengine ukiifungua unakuta message za ajabu ajabu mfano za madada wa pornography wanakuhamasisha uclick ..
Hapo huenda ukisha wahi kutafuta hivyo cookies walitambua hivyo vitu ni moja ya vipendwa vyako.
Ndio maana wanakuletea, huenda si wewe ulie tafuta hivyo vitu lakini simu au kifaa chako kilitumika aubkutumiwa kutafuta.
 
Tumieni Tor browser kwa usalama zaidi
Shida ya hii browser haitunzi kumbukumbu ya tovuti ulizotembelea... Ukiifunga ukafungua unaanza upya... Ikaa muda bila kuitumia let say nusu saa, basi history yote ipo cleared... Sometimes inahitaji ile human verification sijui kila wakati... Na kama una mtandao ambao upo slow huwezi enjoy hii browser
 
Kiukweli hakuna mtu ambaye yuko salama mtandaoni. Awe ni mtaalamu wa ICT au mtu wa kawaida, maadam tu anatumia vifaa ambavyo hajavitengeneza yeye. Hata mitandao mingi tunayotembelea inahusika mno na kutudukua na kufuatilia tunafanya nini mtandaoni.

Binafsi kudululiwa siogopi kwasababu sina la kuficha. Eti nianze kuhangaika na VPN kisa tu naogopa mitandao nayotembelea itafuatilia na kufahamu kwamba nimetoka kutembelea tovuti za ngono au mawasiliano yangu yakoje na watu. Huu mzigo wa kutoyaishi maisha yangu kisa kumuogopa mtu nisiyemfahamu siwezi kuubeba.

Japo binafsi, naona hakuna tabia ya kishenzi kama kudukua taarifa za mtu mtandaoni, kama wewe hauko kwenye taasisi za usalama ambazo zimepewa mamlaka kufanya hivyo kwasababu ya usalama. Yaani ni tabia ya kishenzi mno.
 
Back
Top Bottom