Zaidi ya Watu Milioni 11 wamejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, BVR

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,902
2,000
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.
 
Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,545

hapo bado dsm na mikoa mingine mingi, ina maana wapiga kura tz ni asilimia zaidi ya ngapi? watu tupo 50m, wapiga kura pengine watakua hata 30m kama mwendo ndio huo.
 
Fukara

JF-Expert Member
Dec 28, 2013
1,602
2,000
Mama salma yeye kajiandikisha wapi?au ndio uvumi wa kugombea ubunge Lindi mjini ni kweli..
 
Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,720
2,000
Kwa hali hii CCM inaondoka , maana hawapo kwenye BVR kabisa ....hii ni hamasa ya CHADEMA .
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,991
1,500
Kwa idadi hii napata matumaini kuwa huu mwaka unaweza kuwa wa mabadiliko makubwa.
 
Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Ukawa wajiandae,hii BVR zikiisha andikishwa kura ya maoni ya katiba itaitishwa in short notice.wasijesema hawakujiandaa tu.dalili zote CCM na JK watataka kuipitisha katiba wakiwa na upper hand.unless something changes.
 
Mssesejunior

Senior Member
Nov 21, 2014
130
0
Inawezekana watu wakaandikishwa hata

mil 25 lkn je watapiga kura siku ya uchaguzi?
Kuna mazingira yanaandaliwa yanakayopunguza hio idadi kwa kiasi kikubwa kadir iwezekananvyo.
Moja ya mkakati ni ule wa kuwapeleka likizo wanafunz wote wa vyuo vikuu hivyo watakua likizo japo wamejiandiksha vyuoni. Ndio kusema wale wanatoka mbali na vyuo hawatapiga kura kabisa
 
Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,069

Amini usiamini wanafunzi wengi hawajaandikishwa, kwa mf dar vyup ndio vimefunga jamaa wanarudi mkoa tayari huko maeneo mengi BVR ilishapita
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,915
2,000
Daah!!! Mpaka zoezi likamilike watu zaidi ya milioni 20 wanaweza kuwa wamejiandikisha tatizo watajitokeza kupiga kura?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom