#COVID19 Zaidi ya watu 70% ndani ya Umoja wa Ulaya wamepata chanjo dhidi ya Covid-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja huo umefanikiwa kuwapa chanjo kamili asilimia 70 ya watu ambao ni zaidi ya watu milioni 250 ndani ya Umoja huo. Katika taarifa fupi kwa njia ya video, von der Leyen amesema ni mafanikio makubwa na ya kupigiwa mfano ya Umoja huo kutimiza lengo walilojiwekea la kutoa chanjo ya umma dhidi ya Covid-19.

Rais huyo wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya hata hivyo amewataka watu kuchukua tahadhari kwani janga la ugonjwa wa Covid-19 bado lingalipo, na kutoa wito kwa watu kuchomwa chanjo ili kuepuka wimbi jipya la maambukizo.

Ameongeza kuwa Umoja huo unahitaji kusaidia nchi nyengine kupata chanjo.Kampeni ya chanjo ya Umoja wa Ulaya ilianza katika siku za mwisho za mwaka jana, wakati huo ikilenga kuwachanja asilimia 70 ya watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba.
 
Back
Top Bottom