Zaidi ya watu 100,000 kwenye hatari ya kufa njaa Nigeria

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa zaidi ya watu 100,000 wako hatarini ya kufa kutokana na njaa Katika Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwa sababu ya maasi ya Boko Haram.

Umoja wa Mataifa unasema umeteka nyara sehemu nyingi zilizokuwa zimekaliwa na Boko Haram, lakini ukosefu wa usalama una maana kwamba wakulima hawawezi kuendele na shughuli zao za kupanda.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu milion Saba wanahitaji msaada wa kibinadamau mara moja.

Umetoa wito kwa msaada wa zaidi ya Dola Bilioni moja kupunguza matatizo ya kibinadamu Barani Afrika hii leo.

Chanzo: BBC
 
Nasikia Wole Soyinka kasusa kuishi US simply wamarekani wameamua kumchagua Rais wamtakaye - Trump. Hivi tunavyochangia uzi huu muda huu Soyinka yuko kwenye pipa angani huko akikatisha Atlantic kwa kasi kurudi "nyumbani". Kama hajawahi kula, baadaye leo lazima alishwe mizizi pori - mkataa pema, pabaya panamwita.
 
Hapo ndiyo huwa nashindwa kuelewa Nigeria ni ya pili kwa kwa uchumi barani afrika sasa inakuwaje wananchi wafe njaa?au ndiyo uchumi wa makaratasi
 
Nigeria ni nchi tajiri na ni ya pili kwa uchumi barani afrika kumbe mbembwe tu wananzengo wao wako hatarini kuufukua kwa ajili ya nenge tu
 
Back
Top Bottom