Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
habari ambazo nilizozipata, inahofiwa kuwa zaidi ya watanzania mia moja wamefukiwa katika machimbo ya mererani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini
 
Lini tena hii? Mungu awasaidie wote waliopata matatizo!

Mbona hiyo namba kubwa sana? Ingelikuwa serikali zinazojali watu wake, hata hicho kikao cha Butiama kingeahirishwa.
 
Lini tena hii? Mungu awasaidie wote waliopata matatizo!

Mbona hiyo namba kubwa sana? Ingelikuwa serikali zinazojali watu wake, hata hicho kikao cha Butiama kingeahirishwa.

hii habari waweza kuipata japo kwa ufupi amka na bbc inaonyesha imetokea jana.
 
hii habari waweza kuipata japo kwa ufupi amka na bbc inaonyesha imetokea jana.

Nawapa pole wanaopolo wote waliokumbwa na mkasa Huo. Nilishuhudia yaliyotokea 1997 walikufa zaidi ya 200. kama kuna watu kweli walikua chini (manta wanaita wenyewe) basi uwezekano wa kuwakuta hai ni 0.1%
 
Mungu wetu,ungewachukua mafisadi hata watano,hawa hawana hatia lakini kwa sababu wewe umewapenda zaidi kuliko sisi baba tunaomba uwalaze mahali pema peponi amina.
 
Natoa pole nyingi sana .Naona hata magazeti yetu hayana habari ama waandishi kama kawaida wamejazana Butiama kisa ni vibahasha ?Mungu awarehemu na Mungu uwaangalie jicho baya mafisadi wote hata wakifa basi Mbingu waione kwa mbali sana .
 
Mungu wetu,ungewachukua mafisadi hata watano,hawa hawana hatia lakini kwa sababu wewe umewapenda zaidi kuliko sisi baba tunaomba uwalaze mahali pema peponi amina.

kauli mufilisi... hata hiyo dua yako haina maana tena!
 
Habari muhimu kama hii muwe mnaweka japo link jamani. Wewe umeweka sentensi moja tu kutuhabarisha habari yenye uzito namna hii. Anyway tunashukuru kwa information.
 
Nafahamu vijana hao ni wale ambao hujaribu kutafuta chochote kwa ajili ya maisha yao ya kila siku.

Mipangilio mibovu iliyopo na zana duni ndio vitaendelea kumaliza maisha ya vijana wenzangu na wachakarikaji wengine.

Mwenyezi Mungu awapokee na kuzirehemu roho za vijana hawa waliokuwa maskini.


Kuna mwenye nafasi ya kuhudhuria eneo la tukio na atuletee habari zaidi hapa?

Come on- wana JF wa Arusha!
 
Duh! inasikitisha sana lakini ndio wamejichimbia kaburi la maendeleo ya wachimbaji wote kutokana na swala la safety!
Matokeo kama haya yataleta utata zaidi ktk machimbo hayo ambayo yamekuwa yakitupiwa macho sana na wawekeshaji toka nchi za nje..kwanza wakidai kuwa wototo wadogo wanaopaswa kwenda shule ndio hutumiwa kama watumwa ktk machimbo hayo, sasa tokeo hili linaongeza kuchochea madai yao.
Pamoja na kwamba yawezekana ilikuwa sio makusudio kabisa lakini itaonyesha wazi kuwa machimbo hayo hayana Usalama wa kutosha kuwalinda wachimbaji na kisheria machimbo kama hayo yanaweza fungwa hadi hapo taratibu za safety zitakapo ridhiana na hali halisi ya machimbo hayo.
Kifupi matokeo haya kama serikali itayawekea maanani basi kuna hatari ya machimbo kufungwa....Hizi ni taarifa mbaya sana mbali na kifo cha ndugu zetu 100 ambao nina hakika sababu haikuwa mvua isipokuwa hali mbovu kiusalama ya machimbo yenyewe.
 
Nafahamu vijana hao ni wale ambao hujaribu kutafuta chochote kwa ajili ya maisha yao ya kila siku.

Mipangilio mibovu iliyopo na zana duni ndio vitaendelea kumaliza maisha ya vijana wenzangu na wachakarikaji wengine.

Mwenyezi Mungu awapokee na kuzirehemu roho za vijana hawa waliokuwa maskini.


Kuna mwenye nafasi ya kuhudhuria eneo la tukio na atuletee habari zaidi hapa?

Come on- wana JF wa Arusha!


mafisadi watakuwa wanachekelea mana vijana hawa walikuwa mwiba walisimama kudai haki zao kwa dhati na kila mara ama walipigwa risasi na polisi ama walidhulumiwa hadharani kwa ajili ya kuwapa nguvu wawekezaji na mafisadi .
 
Amen awalaze pema.
Laiti marehemu wangekuwa japo na Bima ili chochote angalau kiwafariji jamaa za wahanga hawa.

Kitu kingine,sikujua kuna tawi au matawi ya vyama humu JF,aiseee!

pole sana kama hukujua hayo.

humu kila mtu ana chama chake isipokuwa INVISIBLE na MODS wenzake tu wao sio wafuasi wa chama chochote.lakin ni watanzania wenye kuipenda kwa moyo wao wote nchi yao,wenye kuitakia mema na kuwatakia mema waTZ wenzao.
 
Kwa mujibu wa http://www.bbc.co.uk/swahili/ Taarifa ya saa 10:00 kwa muda wa Tanzania ni watu wapatao 80 ndiyo wanaohofiwa kufa maji. inasikitisha sana, Kamanda wa polisi anasema kwamba watu hao walitarajiwa kutoka mashimoni leo asubuhi. Wenzao walipo kwenda eneo la tukio walikuta maji yamejaa pomoni. kwasasa wanapump maji ili waweze kuingia ndani. kamanda wa polisi ameahidi kutoa taarifa rasmi baada ya nusu saa.
 
admin WEKA STICKY HII

sioni sababu gan habari za mkutano wa CCM ziwekwe mbele huku watu wamekufa kiasi hiki
 
Watanzania poleni sana na msiba huu; hii dunia sote ni wapita njia na Mungu Mwenyezi ndiye anajua namna tutakavyorejea kwake.

Ajali kama hii ilitokea miaka 10 iliyopita hukohkuo Mererani na inaelekea watawala wetu hawakujifunza kutokana na janga hilo.

Baadaye viongozi wetu kama kawaida yao wataunda tume; itaaandaa ripoti, wataiwasilisha kwa Bwana Mkubwa kwa 'mbwembwe' halafu itawekwa kwenye kabati pamoja na nyingine kama hizo; mfano: ajali ya Mv Bukoba, ajali ya Treni dodoma, ... etc. na hatutakumbuka hadi janga jingine litokee tena!

Hiyo ndiyo Bongo!!!


Sunday, April 12, 1998 Published at 09:40 GMT 10:40 UK
World: Africa
More than 100 feared dead in Tanzania mine floods

_77393_tanzania300.gif

State radio in Tanzania says more than 100 gold diggers are feared dead after heavy rains flooded mines in the north of the country.

The radio quoted the governor of the Arusha region Daniel Ole Njoolay as saying that more than 14 small mines around Mirarani had been inundated; rescuers had so far managed to recover only two bodies.

Mr Njoolay said the local police, fire brigade, a regional water engineer and mines officer were working together to assist rescue operations.

"Rescuers are finding it difficult to go through because of flooding. We are also poorly equipped," he told reporters.

The Tanzanian Prime Minister Frederick Sumaye is expected to fly to the area on Sunday.

The pits in the area are worked by small-scale miners looking mainly for gold and precious stones, including Tanzanite, a semi-precious stone found only in the country.

BBCNews Africa
 
admin WEKA STICKY HII

sioni sababu gan habari za mkutano wa CCM ziwekwe mbele huku watu wamekufa kiasi hiki

hii ni habari nzito sana kwa taifa letu na ilitakiwa ipewe uzito inayostahili, lkn baada yake hata breaking news imeondoshwa.

kulikoni mkuu invisible hebu tujuvye mkuu.

tuwaombeeni dua marehemu (au tujwasalie) mola awapumzishe pahala pema huko mbinguni
 
Back
Top Bottom