Zaidi ya wanyamapori 100 wakiwemo nyumbu na swala wamekufa kwa ugonjwa wa Kimeta

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
kimetaaaaa.jpg


Zaidi ya wanyamapori 100 wakiwemo nyumbu na swala wamekufa kwa ugonjwa wa Kimeta huku serikali ikiwatoa hofu wafugaji juu ya uvumi wa uwepo wa ugonjwa wa Sotoka.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma za mifugo wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi Bw Joramu Mbwira ametoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa sasa umeshadhibitiwa na kuhusu ufafanuzi juu ya ugonjwa wa Sotoka amesema haupo na ni uzushi uliotolewa na kiongozi mmoja huko nchini Kenya.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo maabara kuu Dkt. Henry Magwisha amesema changamoto inayowakabili ni ukosefu wa vifaa ambapo kuna baadhi ya sampuli wanalazimika kuzipeleka nje ya nchi.

Chanzo: ITV
 
Niliisikia hii habari kwa mara ya kwanza kupitia BBC dira tv juzi nilishangaa sana, vyombo vya hapa ni habari za kina nii..
 
Back
Top Bottom