Zaidi ya wanunuzi wa viwanja 30 vya Valenska wilayani Arumeru wadai kutelekezwa na surveyor wa halmashauri

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
490
763
Leo takribani wanunuzi 30 wa viwanja vya makazi na mashamba yaliyopimwa na halmashauri ya Meru mkoani Arusha katika eneo la Valenska karibu na Dolly Estate wamejikuta wametelekezwa na surveyor wa halmashauri hiyo.

Siku kadhaa wakazi wa mkoa wa Arusha waliolipia viwanja katika eneo la valenska walitumiwa ujumbe wa simu kutoka halmashauri ya Meru kuwa leo tarehe 5 September,2022 kuanzia asubhuhi waende kuoneshwa viwanja vyao ili waweze kuchukua hati miliki zao.

Wananchi waliitikia wito tangu asubuhi na walipofika eneo la tukio wakaanza kupigwa danadana mara ooh baadhi ya watu ramani zao zimesahaulika ofisini, oooh mara surveyor yuko mmoja tu wa kuwatembeza wananchi hao.

Wengine wakidai oooh kuna watu wamepimiwa viwanja kwenye nyumba za watu.

Na wengine walisikika wakisema watakiwasha hadi kwa mkuu wa wilaya kwa kuwa walijua kuwa hawana watumishi wa kutosha ni kwanini wawaite watu wengi kwa pamoja?

Wengine walisikika wakisema kuwa masaveya wanataka kuanza mchezo mchafu wa kutaka wanunuzi wawalipe fedha ndio wakawaoneshe watu viwanja, na kuna mama mmoja alisikika akisema alimpa surveyor hela ili akanoneshwe kiwanja.

Ushauri: Halmashauri ya Meru next time mnapoita watu mjipange na msiite watu wote kwa pamoja kwa kuwa hamna watu wa kutosha wa kuwatembeza au kama vipi muazime surveyor kutoka wilaya za jirani.

Mkuu wa wilaya ingilia kati suala hili muda si mrefu litaweza chafua hali ya hewa.
 
Back
Top Bottom