Zaidi ya wanafunzi 3,000 wamekosea kutuma maombi TCU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya wanafunzi 3,000 wamekosea kutuma maombi TCU

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Bilionea Asigwa, Jun 27, 2012.

 1. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imesema kuwa wanafunzi 3,000 kati ya takriban 40,000 waliomba kujiunga na vyuo mbalimbali nchini, wamekosa udahili kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali.

  Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Sifuni Mchome, aliliambia gazeti la MWANANCHI kuwa wanafunzi 37,000 walituma maombi yao kwa usahihi kupitia mfumo unaojulikana kama 'Central Admission System'.

  "...niliangalia na kuona wanafunzi 40,000 wamefanya maombi, hao 3,000 ndiyo wenye makosa mbalimbali (kwa mfano), wengine wameingia tu na kufikiri ndiyo wameshafanya maombi (kuna) na makosa mengine..." alisema Profesa Mchome na kuongeza: "Barua pepe ambazo zitakuwa zimewarudia ni vyema wakazifanyia kazi kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Juni 30, (2012)."

  Alisema kuwa Julai 6, 2012, TCU itakutana na vyuo ili kupitia majina ya waombaji ambapo Julai 15 watakaa na kufanya udahili kamili kwa kuwapangia wenye sifa kwenye vyuo walivyoomba, "Nawaambia wanafunzi wasubiri huo udahili wa Julai 15," alisema Profesa Mchome.

  Katika hatua nyingine, Wakuu wa vyuo na wadau wengine wa Vyuo Vikuu, walikutana jana jijini Dar es Salaam kujadili mfumo wa pamoja wa tuzo (University Qualification Framework). Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kujadili mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Selestine Gesimba, alisema mfumo huo utasaidia kuweka viwango sawa vya mafunzo yanayotolewa na vyuo vikuu vyote nchini.
  NB
  DEADLINE YA KUFANYA MAREKEBISHO NI TAREHE 30 JUNE 2012 KAMA UNA DOGO MWAMBIE ACHUNGULIE ASIJE KOSA CHUO
  SOURCE:GAZETI LA MWANANCHI
   
 2. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Duuuu janga lingine tehama hatujui nani alaumiwe.
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  serikaili inakurupuka kuingiza vitu ambavyo bado haijajipanga navyo ndo athari zake hizi
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana, nimeshuhudia waombaji wengi wakiomba msaada kusaidiwa kujaza maombi kwa wahudumu wa internet cafe, sinauhakika hao wahudimu wanauelewa kiasi gani juu ya jambo hili. Ni wakati muafaka sasa kwa shule zote kuwa na session ya kuwajuiza vijana namna ya kutuma maombi kabala hawajaomdoka mashuleni.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  nakumbuka mimi wakati tunamaliza form six walipita watu kwenye baadhi ya mshule lakini zilizkua sule za mjijini tuu..sasa sijui hata kama huu utaratibu bado upo au ndio mbwembwe za serikali yetu

  HALAFU cha ajabu hao wahudumu wa internet cafe wengi wao ni form four ambao hata TCU wanaisikia kwa wateja wao na hawajui nini kinachoombwa sasa kwa nini watumike kutoa msaada wakati hawajui wanachosaidia???
   
 6. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  chonde chonde tcu waongeze muda watu wafanye marekebisho - mbona wao tcu wameendelea kuifanyia marekebisho system yao hadi majuzi tu baada ya kuona msululu wa wadahiliwa ofisini kwao wakitoa malalamiko kadha wa kadha. hadi leo na saa hii "CHECKING IN PROGRESS" inaendelea kuduwaa takriban wiki sasa na kuwaacha wadahiliwa njiapanda
   
Loading...