Zaidi ya wanafunzi 2000 Ilemela Mwanza wanakaa chini

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Zaidi ya wanafunzi 2000 Ilemela Mwanza wanakaa chini

Zaidi ya wanafunzi 2000 wa shule za msingi katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wanakaa chini kutokana na shule hizo kukabiliwa na ukosefu wa madawati.

Wanafunzi 600 ni kutoka shule mbili za Kayenze na Chasubi ambao wanakaa chini kutokana na ukosefu huo wa madawati.

Pamoja na hilo wilaya ya Ilemela kuna ukosefu mkubwa wa walimu unaosababisha watoto kukosa baadhi ya masomo jambo linarudisha taaluma nyuma.

Ukosefu wa madawati katika wilaya hiyo ya Ilemela ulibainishwa na afisa elimu wa kata ya Kayenze Charles Yohana na afisa elimu wilaya ya Ilemela, ambao wote wawili walielezea changamoto hizo.

Afisa elimu kata ya Kayenze, amesema kuwa shule ya msingi Kayenze ina upungufu wa madawati 164 huku Chasubi ikiwa na uhaba wa madawati 40.

Afisa elimu wilaya ya Ilemela, amedai kuwa katika wilaya yake kuna upungufu mkubwa wa madawati na kusababisha wanafunzi wengi kukaa chini na kueleza pia miundombinu ya vyumba vya madarasa sio rafiki.

Changamoto hizo zinakuja ikiwa tayari Mbunge wa jimbo la Ilemela Angelina Mabula amekuwa akiendesha kampeni kupitia taasisi yake ya "Angeline Foundation" kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa fedha za kununua madawati.

Fedha za harambee kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa madawati na mambo mengine hazijatumika kwa kazi hiyo.

Kampeni hiyo ya kusaidia upatikanaji wa madawati ilianza tangu mwaka 2017 lakini mpaka sasa Mbunge huyo na taasisi yake hawajafanikisha suala hilo.

Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa ardhi nyumba na makazi, amechangisha fedha hizo ambazo inadaiwa zilimsaidia kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020.

Mmoja wananchi wa Ilemela akiwemo, Marco John ni miongoni mwa wakazi wa Ilemela ambao walishawahi kuhoji matumizi ya fedha hizo.

Wananchi wa Ilemela wamekuwa wakihoji kuwa, matumizi ya fedha hizo na kwamba tangu fedha hizo zichangishwe kutoka kwa wadau mbalimbali hazileta manufaa.

Kutokana na uhaba wa madawati unaosababisha wanafunzi kukaa chini, wananchi wanataka fedha zilizochangishwa kupitia taasisi hiyo, zisaidie kununua madawati.

MWISHO
 
Back
Top Bottom