Zaidi ya Wafanyabiashara 1000 kupata nafasi litakapo kamilika soko la kisasa Njombe

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
321
250
1550773404465.jpeg


Zaidi ya wafanyabiashara 1000 halmashauri ya mji wa Njombe wanategemea kupata fursa ya vibanda katika jengo jipya na la kisasa linalojengwa mjini Njombe.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo linalojengwa soko hilo,mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwirn Mwanzinga amesema soko hilo litakalo kuwa na ghorofa moja linaweza kuchukuwa miezi nane kukamilika kutokana na mda aliopewa mkandarasi wa soko hilo huku gharama ya ujenzi huo ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 9 ya fedha za mkopo kutoka benk ya dunia.

“huu mradi tumeanza nao mwezi wa kumi na mbili ambao inatakiwa uchukuwe miezi nane kukamilika kama mkataba unavyosema lakini inawezekana tusifaulu kwa miezi hiyo kwakuwa wakati tunaanza tayari tulikuwa tunaingia katika kipindi cha kifuku ila kwa kifupi tunakwenda vizuri kama mnavyoona mkandarasi yupo vizuri na amejipanga kazi inakwenda katika viwango licha ya kuwa na hii mvua”amesema mwenyekiti Mwanzinga

Aidha amesema kuwa kutokana na changamoto mbali mbali endapo itashindikana kukamilika kwa wakati waliopewa serikali haitasita kumuongezea muda mkandarasi.

“Ni imani yangu tutajitahidi kabisa waende kwa miezi hiyo nane na kama itashindikana basi kutakuwa na kipindi cha ongezeko, na huu mradi ndani tutakuwa na eneo la meza pamoja na eneo la vibanda na shughuli zingine zote zilizokuwa awali zitarudi hapa kama tutakosa sana basi ni bucha ndio zitakosekana kwa kuwa chini na juu kote kutakuwa na meza pamoja na maduka”aliongeza Mwanzinga

Kwa upande wake msemaji wa kampuni ya ujenzi ya Nandura gng & construction co.ltd Lalir Kumar Jangir amesema miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa vifaa kama kokoto lakini haviwezi kupunguza kasi yao ya ujenzi.

“Saizi kipindi cha mvua lakini pili ni upatikanaji wa kokoto hii kidogo ni changamoto na mradi huu tulikabiziwa tarehe 17 julai 2018 na tunatakiwa kumaliza 17 machi 2019 sisi tunaenda vizuri kama mnavyoona isipokuwa kama tutachelewa basi tutaomba mda wa ziada”alisema saiti meneja Lalir Jangir

Geophrey Anton na Scola kyando ni baadhi ya wafanyabiashara wamesema kuwa kukamilika kwa soko hilo kutawasadia kupunguza gharama ya kupata fremu nje ya soko,na kupata wateja tofauti na ilivyo sasa kutokana na umbali wa soko lillipo kwa kuwa wateja imekuwa ni ngumu kufika.

Kukamilika kwa soko hilo kutasaidia kubadilika kwa madhari ya mji wa Njombe huku ikiambatana kuongezeka kwa pato la halmashauri kutokana uwingi wa wafanyabiashara watakaoingia katika soko hilo.

IMG_20190221_131614.jpg

IMG_20190221_131627.jpg

#MC.AMIRI/MR MTAANI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom