Hussein Abdallah
Member
- Nov 1, 2006
- 70
- 9
Zaidi ya wabunge 100 wa CCM hawauziki - Msabah
2008-03-28 10:42:04
Na Ahmed Makongo, Bunda
Zaidi ya Wabunge 100 wa CCM wanaotarajia kujitokeza kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, majina yao hayatarudi ili kukiepusha chama kushindwa katika majimbo yao.
Kauli hiyo nzito imetolewa juzi kwa nyakati tofauti na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC), Bw. Salum Msabah, wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho, kwenye mikutano ya ndani, katika kata ya Kibara na Nansimo wilayani Bunda.
Bw. Msabah alisema kuwa tayari makao makuu ya chama hicho wamekwishabaini wabunge hao kuwa wakirudi utakuwa mzigo kwa chama hicho na iwapo watagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2010 majina yao hayatapendekezwa na uongozi wa juu wa chama hicho.
``Hilo makao makuu tumekwishaliona na kweli wabunge zaidi ya 100 majina yao inawezekana yasirudi, kwa kuwa tukiyarudisha inawezekana wakasababisha chama chetu kikashindwa katika majimbo yao. Hata hivyo utakuwa ni mzigo kuwanadi kwa wananchi,`` alisisitiza Bw. Msabah.
Alisema kuwa baadhi ya wabunge hao wamekwisha kuwa kero kwa wananchi kwa kuwa wakichaguliwa hawarudi tena kwenye majimbo yao na badala yake wanakuwa watu wa mijini tu.
Kuhusu jimbo la Mwibara ambalo matokeo yake ya uchaguzi yalitenguliwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza na kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Bw. Charles Kajege, ambaye amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, Bw. Msabah, aliwataka wana-CCM, wote kuondoa hofu kwa kuwa hata uchaguzi mdogo ukifanyika jimbo hilo litarudi CCM.
Alisema kuwa chama chao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini, kimejipanga vizuri na kamwe wapinzani wasifikiri kuwa hata kama uchaguzi mdogo ukifanyika watalipata jimbo hilo .
``Hakuna sehemu CCM itashindwa uchaguzi mdogo bwana, tumejipanga vizuri sana kuhakikisha jimbo hili tunalichukua, uchaguzi mdogo ukifanyika wote tutahamia hapa, atakuja Marecela, nitakuja mimi, atakuja Rais wetu, atakuja mzee Makamba na watakuja viongozi wetu wote... Sasa wapinzani watashindia wapi,`` alisema.
``Na sisi tutafanya kampeni kubwa ya nyumba kwa nyumba, kichwa kwa kichwa, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka...,`` alisema na kushangiliwa na umati mkubwa uliokuwa umehudhuria mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kibara.
Aidha, Bw. Msabah alikiri kuwepo kwa wana CCM., ambao ni wanafiki wanaochangia chama hicho kushindwa katika baadhi ya majimbo, kata, vijiji na vitongoji kwa kuwa wamekuwa hawana msimamo.
Alisema kuwa vyama vya upinzani vilivyoko hapa nchini ni wasindikizaji na kila siku vinazidi kushuka ngazi ya ubora kwa wananchi.
Katika mkutano huo zaidi ya wanachama 60, wa vyama mbalimbali vya upinzani, wengi wao wakiwa ni kutoka TLP, walirudisha kadi za vyama hivyo na kujiunga na CCM.
SOURCE: Nipashe