Zaidi ya vyingine vyote, Vijana tujifunze Miiko ya kujadili Siasa

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Sio mara moja nimepost topic ya siasa inayogusa pande tofauti; na kinacho unganisha pande zote, ni tamaduni mbovu za kukabiliana na mawazo tusiokubaliana nayo.

Hii ni mifano:

1.Ad hominem (Latin for "to the man" or "to the person"),: fallacious argumentative strategy whereby an argument is rebutted by attacking the character, motive

KUMTUSI: MTOA MADA, NIA YA MTOA MADA, LUGHA AU TABIA YA MTOA MADA.
a) Hii si sahihi, ni kinyume cha mwiko wa majadiliano, na inanyima kina maongezi.

3. Tofautisha kati ya : Maoni (opinions) na Ukweli (facts)
Maoni:

kila mtu anayo, yanatokana na mtazamo, hayaitaji upelelezi kutungwa, sio lazima ukubaliane nayo, na kuwa makini ukiyaona (usiamini mpaka upewe ushaidi)

Ukweli (facts)
hii ni mkusanyiko wa mitazamo inayo-suppot-iwa na ushahidi, ushaidi unapaswa kuweza kusimama shangaa kukosolewa, ushaidi unapaswa uwe wazi kwa kila mtu kuuona.
mfano; makaratasi ya kisayansi yaliosimamiwa na wataalamu, video na picha bila edit, maneno ya watu wengi waaminifu na sio mtu mmoja
Tafadhali: hakuna usawa wa ushahidi; wanachosema wanasiasa si ushahidi, mpaka watoe vyanzo vyao!!!!

Ndo maana mtazamo wa mtu mmoja ni anecdote, na wa watu wengi ni takwimu

4. Malinganisho yasiyo sawa
Sio sawa kujibu kila mada kwa kulinganisha madai dhidi ya pande yako na nyingine, hasa hasa ikiwa haipo ndani ya mda

Ovu la mwingine alisafishi ovu lako; Hakuna mahakama inayofuta mashtaka, kisa kosa kufanyika na mwingine nje ya mahakama.
"kila mtu abebe msalaba wake"

5. Heshima kwa watoa hoja
Sio lazima ukubaliane na mtu, ila tambua kwamba fikra ujengwa na tazamo nyingi na sio za mtu mmoja.

Tumia hii nafasi kuelewa pande jilani, na tafuta unachokubaliana, pambana kifikra na usicho kubaliana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom