Zaidi ya ulimbo nitumie mbinu gani nyingine ya kisasa kuwatega ndege wadogo shambani?

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
4,312
5,979
Jamani huko vijijini watu wamekuwa wakitumia ulimbo kuwategea ndege wadogo mashambani au sehemu za vichaka ndege wengi wanapotua. Huo ulimbo unatokana na utomvu mzito wa miti fulani ambao uchemshwa na kupatikana ulimbo ambao uweza kutumika kunasia ndege kwa siku kadhaa.

Sasa mwenzenu nina shamba langu ambapo kuna sehemu italimwa lakini sehemu nyingine ambayo ina vichaka vichaka itabaki hadi hapo baadae. Kila niendapo shambani naona kuna ndege wadogo wadogo ambao huruka kwa makundi makubwa makubwa kiasi na kutua kwenye hivyo vichaka. Kwa uzoefu wangu hao ndege uliwa.

Hivyo napenda kujua kutoka kwenu ni mbinu gani ya kisasa zaidi mbadala wa ulimbo ambayo naweza kuitumia kuwatega hao ndege wadogo wadogo kwa usalama na kuniwezesha kupata kitoweo na hivyo kunifanya niongeze upendo kwenye safari zangu za kwenda huko shambani. Je, huko kwenye maduka ya kilimo na mifugo naweza kupata vifaa vya kuwatega?
 
Nenda U-tube, kuna mitego kibao ya ndege wanaelekeza jinsi ya kutega. Hata ukitaka kumnasa mamba mitego ipo tena simple tu
 
Chukua pumba changanya na gongo weka kwenye chaka lao, wakishuka kwenda kula subiria tu kidogo unaenda waokota kama embe vile...
 
Jamani huko vijijini watu wamekuwa wakitumia ulimbo kuwategea ndege wadogo mashambani au sehemu za vichaka ndege wengi wanapotua. Huo ulimbo unatokana na utomvu mzito wa miti fulani ambao uchemshwa na kupatikana ulimbo ambao uweza kutumika kunasia ndege kwa siku kadhaa.

Sasa mwenzenu nina shamba langu ambapo kuna sehemu italimwa lakini sehemu nyingine ambayo ina vichaka vichaka itabaki hadi hapo baadae. Kila niendapo shambani naona kuna ndege wadogo wadogo ambao huruka kwa makundi makubwa makubwa kiasi na kutua kwenye hivyo vichaka. Kwa uzoefu wangu hao ndege uliwa.

Hivyo napenda kujua kutoka kwenu ni mbinu gani ya kisasa zaidi mbadala wa ulimbo ambayo naweza kuitumia kuwatega hao ndege wadogo wadogo kwa usalama na kuniwezesha kupata kitoweo na hivyo kunifanya niongeze upendo kwenye safari zangu za kwenda huko shambani. Je, huko kwenye maduka ya kilimo na mifugo naweza kupata vifaa vya kuwatega?
Tengeneza tundu kubwa ambalo ndege akishaingia,kutoka hatoweza. Nakumbuka kipindi nipo mdogo huko kijijini babu alikua anarudi na ndege wengi sana zaidi ya 200 kila siku na walikua hawaishi. Alikua anatumia tundu la kutegea ndege,ndani ya tundu alikua anaweka mtama
 
Hilo tundu linatengenezwaje hadi ndege washindwe kuruka na kutoka?
 
Chukua pumba changanya na gongo weka kwenye chaka lao, wakishuka kwenda kula subiria tu kidogo unaenda waokota kama embe vile...
Kabla sijawanasa hao ndege nitakuwa nimenaswa na vyombo vya dola kwa kukutwa na gongo ambayo kwa sheria za nchi ni kinywaji haramu.
 
Back
Top Bottom