- Thread starter
- #21
Mambo mengine hata kuanza kuyafikiria ni aibu. Lakini pia yanatudokeza mambo mengine ambayo yameendelea baadaye. Kuna watu siku moja watatakiwa kujibu walipolifikisha taifa hili hapa.
Kuna mapungufu makubwa sana ya 'thinkinig' katika safu ya political elite hapa nchini. Hii cable inaonesha ni jinsi gani wakubwa wanashindwa am kuungaisha dots au wamedhamiria kuwa 'darling' wa nchi zingine. Tanzania sasa hivi inapiganiwa na nchi za kadhaa zenye mrengo tofatuti. Lakini Marekani na Wachina na Canada ndio vinara wa kuchanja mbuga. Kupita American Peace Corps, hawa wakubwa wametuma utitiri wa watu wao. sasa hivi wako kila mahali, kuanzia Kigoma, mpaka Arusha. Mafunzo ya kijeshi nayo yanaendelea both marekani na wachina.
Na swali nilalojiuliza bila kupata jibu hata kidogo ni hili; viongozi wetu wanafanya haya yote kwa sababu wanataka kujenga Tanzania ya namna gani?