Zaidi ya sh milioni 10 zatengwa kufuturisha mkoa wa Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya sh milioni 10 zatengwa kufuturisha mkoa wa Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  SUNDAY, JULY 22, 2012


  [​IMG]

  Zaidi ya sh milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kufuturisha watu
  wenye kipato cha chini kwenye mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.


  Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaa leo,
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madina, Sheikh Ally Mubaraka alisema hayo wakati alipokuwa akipata futari kwa pamoja na waislamu wa Msikiti wa Sheikh Gorogosi, Tandika kwa Maguruwe.

  Alisema fedha hizo zimepatika kutokana na ushirikiano mzuri
  uliyopo kati ya Ubalozi wa Emirate na taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji
  misaada katika jamii yenye mahitaji maalum.


  Sheikh Mubaraka alisema taasisi hiyo inalenga kutoa futari
  kwenye makundi ya watu ikiwa ni ishara ya huruma kama dini hiyo inavyoelekeza.
  "Ubalozi wa Emirate umejitolea fedha za kutosha kwa ajili kufuturisha
  ambapo leo (jana), tumeanzia Tandika, mpango huu ni wa kila mwaka na utafika
  katika maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam"alisema Sheikh Mubaraka.


  Sheikh Mubaraka aliwaasa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei
  za bidhaa kwa ajili ya kujipatia kipato kikubwa ambapo sheria za dini zinawataka
  wanadamu kuoneana huruma wakati wote.


  Vilevile alisema mwezi huu wa mfungo Ramadhani ni fursa njema ya kufanya ibada kitendo ambacho kitawasidia waislam kufutiwa dhambi zao.


  "Yule mwenye kula mchana katika mfungo huu,hata kama atakuwa akijibidiisha na swala atambuwe kuwa hatoweza kufutiwa dhambi zake"alisema Sheikh Mubaraka.


  Akizungumzia tukio la kuzama kwa meli ya Skagit, alisema taasisi hiyo imetoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao kwani tukio lile ni kubwa ambapo uchungu wake umemgusa kila mtu katika nchi hii.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Good... Itasaidia Wananchi wasio na Uwezo

  SUNDAY, JULY 22, 2012

  [​IMG]
  Zaidi ya sh milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kufuturisha watu
  wenye kipato cha chini kwenye
  mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar
  es Salaam.

  Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaa leo,
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madina, Sheikh Ally Mubaraka alisema hayo wakati alipokuwa
  akipata futari kwa pamoja na waislamu wa Msikiti wa Sheikh Gorogosi, Tandika kwa Maguruwe.

  Alisema fedha hizo zimepatika kutokana na ushirikiano mzuri
  uliyopo kati ya Ubalozi wa Emirate na taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji
  misaada katika jamii yenye mahitaji maalum.


  Sheikh Mubaraka alisema taasisi hiyo inalenga kutoa futari
  kwenye makundi ya watu ikiwa ni ishara ya huruma kama dini hiyo inavyoelekeza.
  "Ubalozi wa Emirate umejitolea fedha za kutosha kwa ajili kufuturisha
  ambapo leo (jana), tumeanzia Tandika, mpango huu ni wa kila mwaka na utafika
  katika maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam"alisema Sheikh Mubaraka.

  Sheikh Mubaraka aliwaasa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei
  za bidhaa kwa ajili ya kujipatia kipato kikubwa ambapo sheria za dini zinawataka
  wanadamu kuoneana huruma wakati wote.

  Vilevile
  alisema mwezi huu wa mfungo Ramadhani ni fursa njema ya kufanya ibada kitendo
  ambacho kitawasidia waislam kufutiwa dhambi zao.

  "Yule mwenye
  kula mchana katika mfungo huu,hata kama atakuwa akijibidiisha na swala atambuwe
  kuwa hatoweza kufutiwa dhambi zake"alisema Sheikh Mubaraka.

  Akizungumzia
  tukio la kuzama kwa meli ya Skagit, alisema taasisi hiyo imetoa pole kwa
  familia zote zilizopoteza ndugu zao kwani tukio lile ni kubwa ambapo uchungu
  wake umemgusa kila mtu katika nchi hii.
  [/QUOTE]
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hizi nazo ni habari za siasa??
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Itasaidia sana sana kwa wenye kipato haba...ila tu imani itumike zaidi maana mwisho siku isije kuwa kashfa!ni mawazo na tahadhali tu
   
 5. escober

  escober JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sasa mkuu hii nayo ni habari ya siasi au you are just seeking peoples attention
   
 6. E

  Eddie JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole Nguu007 naona ulitaka wagala wenzie waka support kuponda Uislam lakini wamekugeuka, jipange upya uje kivingine hii hailipi!
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  naam ndio philosophy nzima nyuma ya funga ... kulisha wasiojiweza na kutoa sadaka!
   
 8. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo nafasi ya wanasiasa kuuza sura sasa huko Magazetini, hasa wale wa chama tasa. mimi nauliza kama hawa Imarati wana pesa na nia kweli ya kufuturisha, kwanini wasifuturishe Tanzania nzima? kwanini wanabagua mikoa mingine, au dar es salaam tu ndio kuna waislamu
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nchi yetu kwasababu ya Matajiri Uchwara GAP ya walio nacho na wasio nacho imeongezeka kuliko miaka 30 iliyopita
  Hii ya Mkoa wa Dar kuweka akiba ya Milioni 10 ni ya kuvutia; lakini ni Mkoa Mmoja tu na huu mkoa ni tajiri

  Kuna Mikoa Ambayo kuna Watoto na Vijana wa kiislamu hawawezi kufuturu sababu tu hawana uwezo lakini wanataka
  kufuata nguzo zao za kiislamu; kama Mkoa wa Shinyanga, Mwanza, Sumbwanga hiyo Mikoa pia itoa fedha kama Dar

  Na isaidie; wewe acha nuksi zako Usidhani Mimi nina Mawazo finyu ka UDINI kama wewe... nawaza Maendeleo

  Ya wanadamu wenzangu
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nyie sababu Mawazo yenu finyu; Niliona huu ni Mwamko mzuri sio kwa Mkoa wa Dar pekee; kuna Mkoa wananchi wake

  Masikini zaidi ya Dar; wangefanya kama Dar ili kusaidia wananchi... Wewe kama unajiweza hongera Usinipe pole mimi

  Jihurumie wewe usie na Moyo wa kutoa
   
 11. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Natumai walengwa watafikiwa, ila ni bora kuwawezesha watu waweze kusimama wenyewe kuliko kusubiri kuwapa futari.
   
 12. E

  Eddie JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa ulitaka Dar wasiftarishe mpaka mikoa yote iwe na futari? Udini umekuzidi mpaka unaweka masuala ya futari kwenye siasa
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah Ni Siasa Mkoa Mmoja Umetoa Msaada; wapi Mikoa Mingine?
   
 14. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  nawe unapotosha, ni mkoa mmoja, au tandika kwa maguruwe tu?. kama nimetafsiri vibaya nisamehe mkuu
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  * UMESOMA BILA KUELEWA ANGALIA CHINI
  Zaidi ya sh milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kufuturisha watu
  wenye kipato cha chini kwenye
  mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar
  es Salaam.
   
 16. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  View attachment 59562  natoa pongezi kwa waliofanikisha zoezi.
   
Loading...