Zaidi ya ndoa 365 zimevunjika Temeke (Dar es Salaam) tangu mwaka 2021

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
ndoooaaaaaaaaa.jpg
Zaidi ya ndoa 365 zimevunjika katika Manispaa ya Temeke katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi Julai 2022.

Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Temeke, Lilian Mafole na kusema chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo ni mifarakano, wivu wa mapenzi na kipato duni.

Afisa Ustawi amesema kutokana na ndoa hizo kuvunjika watoto wamekuwa wakiteseka kwa kukosa malezi na hatimaye watoto hao kujikuta wakifanyiwa ukatili wa kingono kutokana na kutokuwa na malezi bora kutoka kwa wazazi wa pande zote mbili.


Chanzo: Eatv
 
Mpaka jeshi la polisi kupitia maafisa kusema "badala ya kung'ang'ania kukaa na mtu anayekutesa na kukufanyia unyama bora uondoke, kwani hamkuzaliwa naye... "

Yasije kukukuta ukiwa haupo duniani na kuacha majonzi ni bora kuondoka uanze maisha mapya".

Kutokana na madawati ya jinsia kutoa ushauri wa ajabu wa kutengana, hizo 365 ni Ndoa chache sana na bado sana.
 
1. Ndugu kuingilia ndoa, za wana ndoa
2. Mume/Mke kushindwa kusimama kwenye wajibu na majukumu yake
3. Matatizo ya kiuchumi
4. Ongezeko la mafunzo toka kwa wanaharakati

Ndio sbabu kuu za kuua ndoa kwa miaka ya karibuni.

Madhara:

Tangu ndoa kuwa muunganiko wa watu wawili kihisia, kimwili na kiakili, majeruhi wa kwanza kwenye anguko la ndoa ni wanandoa wenyewe. Na wana athirika kihisia, kiakili na kimwili (Kiasi kwamba kuingia kwenye mahusiano na mke/mume walio talikiana, unahitaji ujipange).

madhara mengine:

  1. Kufa kwa urafiki na Undugu,
  2. Kuyumba kwa uchumi na Maendeleo ya mwanandoa
  3. Kuathiri makuzi na malezi ya watoto kiakili, kimwili na kiimani
Suruhisho: UJIO WA NDOA ZA MKATABA
 
Back
Top Bottom