Zaidi ya Migodi 15 Merereni yateketea kwa moto Arusha

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,480
907
Migodi midogo 15 ya wachimbaji madini wadogo wa madini imeteketea kwa moto katika Eneo la kitalu B Mirerani simanjiro Chanzo kikiwa ni hitilafu ya umeme wakati mafundi walipokuwa wakitengeneza moja ya mita iliyokuwa katika moja ya nguzo zilizokuwepo eneo hilo na inagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4.

Zaidi ya watu 1000 wanakosa makazi baada ya migodi hiyo kuungua Moto.

Chanzo: ITV Breaking News
 
NAAMINI WAKENYA WAMEUMIA ZAIDI KULIKO WATANZANIA JAPO MIGODI IYO IKO TANZANIA. EEEEh ASANTE BWANA
 
Sasa kama taarifa ya jana ilitaja migodi 7 na leo ikaongezeka hadi kufikia 15 isitangazwe?

Kaka niko eneo ambalo ndio imetokea ajali mgodi we2 ni wa mwisho kabisa kwa kwenda juu,migodi ni 7 tu hiyo mingine huyu mwandishi ni muongo,pia ni migodi ya wachimbaji wadogo sio tanzaniteone kwa kaburu
 
Kwa hiyo ITV ni waongo! Wamepata wapi hizo taarifa? Kama si kweli mbona serikali haijakanusha!
 
Jumla ambayo imeteketea kabisa ni 8 pamoja na miwili ambayo imeungua kiasi ila hasara ni kubwa sana unakuta mtu mgodi mpka ukae sawa umetumia 500m wengine mpka 1bn kutokana na miundo mbinu yako,kwa kipindi hiki bei ya tanzanite iko juu lakini madini yanatoka migodi michache 2 kwa kiwango kidogo
 
Kwa hiyo ITV ni waongo! Wamepata wapi hizo taarifa? Kama si kweli mbona serikali haijakanusha!

Ngoja niweke sawa migodi iliyoteketea na majina yake,titanic,kwa wapendwa,john jungle,kwa muhindi,mama pili,kwa nene, hiyo ndio imeteketea kabisa wengine waliwahi zima moto pia upepo n ukaribu ya mgodi na mgodi ndio umechangia moto kusambaa kwa haraka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom