Zaidi ya madereva 300,000 wabadilisha leseni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya madereva 300,000 wabadilisha leseni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Feb 20, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga


  Madereva zaidi ya 357,552 wamebadilisha leseni zao za zamani na kupata mpya tangu zoezi hilo lilipoanza Oktoba mwaka 2010.
  Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alisema zoezi hilo linaenda vizuri kwa kuwa waliobadilisha leseni ni nusu ya lengo.
  "Hadi sasa madereva wapatao 357,552 wamebadilisha leseni zao na hili zoezi linaenda vizuri tangu lilipoanza oktoba 2010," alisema Mpinga.
  Alisema zoezi hilo limeenda vizuri baada ya operesheni waliyoifanya januari mwaka huu kwa madereva wa mabasi yanayobeba abiria wengi wao wameitikia wito na kwenda kusoma ili waweze kupata leseni daraja C.
  Alisema kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita kulikuwepo na msongamano katika vituo vya kukatia kwa kuwa mtandao ulikuwa chini ikawalazimu kuagiza wataalamu kutoka Israel kutatua tatizo hilo na kwa sasa zoezi linaendelea kwa kasi.
  Mpinga alitoa wito kwa madereva ambao hawajabadilisha leseni zao wafanye haraka kufanya hivyo hasa kwa wale wa daraja C kwa kuwa wasipofanya hivyo watakakosa sifa za udereva kuendesha magari ya abiria.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  wamekusana, fungu la nguvu!
   
 3. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Yaani muda woote huo tangu waanzishe huu utaratibu ni watu laki tatu na tu!
  Jamani Bongo kweli waachie wabongo wenyewe hakuna kitu kinafanyika na kufanikiwa
   
Loading...