Zaidi ya billion 3 za machinjio ya kisasa zayeyuka Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya billion 3 za machinjio ya kisasa zayeyuka Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dosama, Mar 28, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Zaidi ya shillingi za TZ billion tatu zilizotengwa kwa ajili ya kujenga machinjio ya kisasa jijini Dar yameyeyuka pasipo majibu mara baada ya kamati ya bunge ya serikali za mitaa mh Agustine Mrema kubaini ufisadi huo. Dr Masaburi nae adai kuna vifaa vilikuwa vitoke Austrilia ila havijafika.

  Swali kama vifaa vya Austrilia mbona hakuna viambatanisho kuonyesha kama kuna invoice na malipo yalivyofanyika?
  Hivi hawajulikani walio kula au ndo walewale niguse uone

  Source star tv habari
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimeshtushwa zaidi na majibu ya Mayor Dr Masaburi kwamba kampuni iliyokuwa inahusika IMEFILISIKA kabla haijakamilisha kazi! Huu ni mchezo ulioota mizizi hapa nchini kwa makampuni kuchukua tender wanapata pesa halafu ghafla wanafilisika!

  Kwenye hili ni vizuri jina la kampuni na wakurenzi wake yawekwe wazi ili wananchi wawatambue. Bilioni 3 ni hela nyingi sana haiwezekani Mayor atoe maelezo rahisi na watu wakubali.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwamba imefilisika? Hii kitu haiwezekani hasa inapokuja biashara ya nje unalipaje? Unalipa upfront au against bill of lading? Billion 3 siyo hela fupi ya kusema kirahisi kwamba kampuni imefilisika. Hawakufanya due diligence, hawakupata performance Guarantee? Unalipa 100% kweli kabla hujapata mzigo? Hakukuwa na letter of credit?

  Watu wasitake kutufanya sisi majuha. Kuna scheme ya watu kuanzisha vikampuni na kujichukulia pesa za serikali na kisha kujifilisi. Hata wakubwa wanajua hili.

  Nimgekuwa na mamlaka ningemwita huyo Masaburi nimhoji na baada ya kumhoji namkabidhi kwa polisi wamfunge pingu na kwenda kumficha bila kumfungulia mashitaka kwanza hata kama ningeitwa dikteta wacha iwe. Watu wanaishi kimjini mjini hapa.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Amwsema Kampuni ikifirisika utamdai nani hakuna wa kumdai,yaani mimi nadhani hiyo kampuni ni yake manake hana mshipa wa huruma wa fedha za walala hoi ,nchi hii viongozi wa ajabuajabu kama Masaburi ni wa kupiga risasi kama Mtikila alivyosema
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sasa unashangaa nini Mkuu, si ndio sera ya kifisadi inayosimamiwa na serikali ya CCM na ambayo wengine tunaipiga vita? Je, uko pamoja nasi?
  FYI hao unaowaita wakubwa ndio wahusika wakuu na huo ndio mchezo wa viongozi wa serikali ya CCM tunaoupiga vita.
  Je uko pamoja nasi?
  Ungekuwa na mamlaka ndani ya serikali ya CCM ungejifungulia mashtaka? Kumbuka uongozi ndani ya CCM hupatikana kwa rushwa! Je, uko pamoja nasi kupambana na huo uovu? Dawa ni kuondokana huu utawala haramu wa CCM.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Masaburi anajibu kiasaburi...mambo gani haya.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi naupinga ufisadi hakuna siku ambayo nimeushangilia ufisadi. Unajua mambo mengine yanakera kwelikweli. Masaburi alipoingia kwenye Umeya nilidhani atafanya vyema kuliko Kimbisa kumbe ameenda kufisadi tu jiji na kutoa majibu ya hovyo hovyo tu.

  Mkuu tupo pamoja katika kupiga vita ufisadi wa aina yoyote unaofanywa na mtu yeyote toka chama chochote ama shirika lolote.
   
 8. c

  collezione JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Sasa kama accountants wetu wana_vidiploma vya enzi ya nyerere, kwa nini hela zisipotee.

  Kwa jinsi nilivyosoma thread ya jana. Nina wasiwasi pia na utendaji wa wahasibu wetu... Sidhani kama wana elimu ya kutosha kulingana na dunia ya sasa ya technologia.

  Huwezi amini mtu amesoma diploma enzi ya nyerere afu ndo mhasibu mkuu wizara ya mambo ya ndani...sasa mtu kama huyu ni wazi bado anatumia primitive methods za accounts... Na ndo hapa mafisadi wanachota hela kirahisi. Sometimes ni maksudi au ni uzembe pia
  Unachangia kwenye ufisadi hapa Tanzania.
  Inakuaje mpaka POC wanakuja kugundua. Kwani hizo hela hazina muhasibu??? Yeye muhasibu hawezi shtuka kama hela nilizotoa zimepotea???

  Hivi unadhani, ukienda kwenye international organisations, au nchi zilizoendelea kama UK. Utakuta mhasibu mkuu amekalia kiti chake zaidi ya miaka 6?. Hata kama ni pHD holder, mwenye ufanisi mkubwa wa kazi. Hawezi kukalia kiti hicho hicho zaidi ya miaka 6. Maximum kabisa 8-10. Hapo kweli walimuona jamaa kichwa.

  Hapa kwetu wahasibu wako ofisini zaidi ya miaka 20. Na ki_diploma..

  Duh kweli
  Tanzania ajira ni dhamana ya maisha. na hiyo ndo ina_tucost.

  Mashirika yote ya umma yanakufa kwa sababu ya auditing mbovu.
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  very right, conditions of contract zinahitaji performance bond guarantee and advance payment bond
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  i see........
  ina maana wamechinjia tumboni au?
  bongo bwana kila mahali sanaa............
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jina lenyewe masaburi...

  Wajanja wameshaingiza kwenye miradi yao
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Haya maprado na Vogue mengi yapo barabarani kwa njia za mkato mkato. Huu ni uthibitisho wa jinsi ambavyo nchi hii kujengeka itakuwa ndoto.
   
 13. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Meya: Kampuni imefilisika

  Hata hivyo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi alisema kampuni hiyo imefilisika na kwamba hakuna mtu atakayeweza kulipa deni hilo. Kutokana na hali hiyo, alisema watakaa na halmashauri za manispaa ili kuangalia jinsi ya kutatua matatizo hayo.

  "Kampuni yenyewe imefilisika, nani atalipa deni hilo? Hakuna kwa sababu hata jiji ni miongoni mwa watu waliotapeliwa japo tulikuwa tumeingia ubia lakini kilichofanyika ni kwamba mradi huo haujatekelezeka," alisema Dk Masaburi.
  Alisema machinjio hayo yalitakiwa kujengwa mwaka 2006, lakini mpaka sasa hayajengwa na wala hakuna eneo la ujenzi.
  Meya Masaburi alisema halmashauri hizo zilitoa fedha hizo na kudaiwa kuwa zimetumika kwenye upembuzi yakinifu na kuongeza kwamba, ilipofika mwaka 2009, madiwani wa jiji na manispaa walitaka ufafanuzi kuhusu suala hilo na kuitaka jiji kujiondoa kwenye mkataba huo jambo ambalo lilisababisha halmashauri hizo kudai fedha zao ambazo mpaka sasa hazijalipwa.
  Alisema wakati hayo yakiendelea, tayari kampuni hiyo ilikuwa imefilisika na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuendelea na mkataba au kurudisha fedha.
  "Meneja wa kampuni hiyo ambaye ni raia wa Zimbabwe aliyejulikana kwa jina la Benjamin Chipazi ni miongoni mwa watu waliotapeliwa, anadai mafao yake ya zaidi ya Dola za Marekani 150,000, lakini ameshindwa kulipwa kwa sababu hakuna mtu aliyerithi madeni hayo," alisema.

  Alisema kutokana na hali hiyo, jiji haliwezi kurithi madeni ya kampuni hiyo na kwamba kila mmoja anapaswa kutambua kuwa katika mkataba huo wametapeliwa.

  Source: Mwananchi

  Hivi Kikwete atachukuliana na viongozi wazembe na wezi kama huyu mpk lini? hata mtoto mdogo wa darasa la tano huu utumbo hataukubali....kabla ya kampuni kupewa tender si ni lazima uwezo wake uthibitishwe?....Masaburi rudisha fedha za Watanzania au la... Laana itakuandama wewe na kizazi chako...Umekula UDA hukushiba?? inaniuma sana!
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kuna haja ya kuiba kabla ya ccm kufa ,la sivyo tuchukue sisi cdm wezi waondoke
   
Loading...