Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wednesday, 17 February 2010
Uchunguzi wa awali wa vyanzo vyetu mbalimbali unadokeza kuwa hadi hivi sasa zaidi ya shilingi bilioni 25 za vocha ya manunuzi ya pembejeo za kilimo (hususan mbolea na mbegu) zimetafunwa katika mikoa ipatayo 20 iliyopewa mfumo huo wa ruzuku ya serikali. Watendaji mbalimbali wa serikali kuanzia mkoa hadi vijijini kwa kushirikiana na watumishi wa ngazi mbalimbali wameshirikiana katika kutumia vibaya vocha hizo ambayo karibu nusu ya fedha zilizotengwa katika kusaidia upatikanaji wa zana na pembejeo za kilimo zinaonekana kutumiwa vibaya.
Tangu tuliporipoti juu ya wizi wa vocha za zaidi ya bilioni 7 huko Rukwa uchunguzi wetu wa awali kwa mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Kigoma na Iringa unaonesha kuwa serikali ya Rais Kikwete imejilundikia kashfa nyingine kubwa.
uchunguzi wetu huu wa awali ambao tutaufunua siku chache zijazo unaonesha kwa mara ya kwanza mfumo wa ufisadi umeweza kutawanywa hadi ngazi za chini kabisa ambazo zamani zilionekana kukingwa. Katika mtindo huu wa sasa inaonekana hadi watumishi wa ngaza za chini sana wamehusishwa katika kushiriki katika kufanikisha mtandao wa uchotaji wa fedha hizi kwa kutumia mbinu ambayo imekuwa ikitumika katika manunuzi mengine.
Watu ambao wanaendelea kuumizwa ni wakulima wa kawaida ambao sasa wanataka mbolea (ambayo ipo) lakini hawana vocha za kununulia na hivyo wengine kulazimika kulipia ununuzi wa pembejeo hizo katika bei yake halisi na hivyo kudefeat kabisa lengo zima la vocha.