Zahera na AS Vita ndani ya nchi hii?

Mimi sijaelewa Zahera ana ihujumu vipi Simba kwa kushiriki kwake na timu ya As Vita. Yule sio mtanzania ni mkongo, na ile As Vita ni timu inayotokea Congo, Kocha wa Vital ni kocha mwenzie anayefundisha nae timu ya taifa ya Congo. Tatizo lipo wapi kwa Zahera kumpa mbinu za kiufundi kocha mwenzie? Hapo hakuna hujuma, labda kama Zahera anafanya namna ili marefa wahongwe, au kama anafanya mbinu chafu zisizoruhusiwa kwenye mpira wa miguu. Lakini kama anaisaidia Vita kwenye mambo ya kiufundi kwenye uchezaji wa mpira basi kwa upande wangu sioni hiyo hujuma kwa timu ya Simba.

Na pia Zahera halipwi mshahara na watanzania, bali analipwa mshahara na timu ya Yanga ambao ndio maasimu wa Simba.
Sent using Jamii Forums mobile app
Zahera mwenyewe alishindwa kuifunga Simba SASA anamdanganya nini ibenge???

Acha wanikusanye tuwapige Kwa ujumlaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Zahera ana uhuru wa kuzunguka na AS Vita popote mjini hapa. Si AS Vita tu, hata na Al Ahly au Nkana, hakuna tatizo kwa kuwa huenda ana malengo mapana zaidi kuliko ya kuwa kocha wa Yanga. Lakini ambacho aliharibu (hata kama hakuvunja sheria au utaratibu) pengine ni kusema tu hataenda Iringa kwa kuwa anaenda kwao DRC. Angekaa tu kimya awasubiri AS Vita hapa Dar. Pengine wanamlipa vizuri kuliko Yanga, tumuache tu
 
Write your reply...
mikia fc mshasahau walichokifanya haruna niyonzima na masoud djuma kwenye mechi ya shirikisho yanga na rayon

acheni kulalamika,mutu ya kongo iko mujini
 
wana yanga tupo nyuma ya kocha wetu zahera... simba wanaanzia wapi kuwakilisha nchi..

simba na yanga ni wapinzani wa jadi .. hata siku moja mwana yanga hawezi muombea simba ushindi... zaidi ya unafiki tu..

na ninataka mfungwe 5
Hahahahahahahaha
 
Hizo 5 5imba washazizoea, wagongwe hata 13 tu. Kama waliwaanika waarabu juani, hawa Bana Congo ni Tshishimbi Type, twende jua twende mvua
 
Tumuache Zahera apooze machungu ya Yanga kufungwa na Simba. Pengine atafarijika akiona walau Vita imemsaidia kulipa kisasi
 
Hivi sio vita vya nchi hizi ni timu mbili kutoka mataifa mawili tofauti, hata CAF waliacha utaratibu wa nyimbo za Taifa kwenye mechi za vilabu.
Isitoshe njia za mawasiliano zipo nyingi hata asingekutana nao bado kama kuna vitu vya kuwaambia anaweza kupiga hata simu!!
Najiuliza hivi press conference zetu ni waandishi kusikiliza tu hata kuhoji hakuna maana huyu alitakiwa aambiwe pale pale apunguze ujinga
 
Nimeona Haji akiongea kimafumbo juu ya huyu kocha kuwa alidanganya kwenda Kongo lakini kumbe yupo na AS Vita hapa nchini.

Kama yanayosemwa ni sahihi basi huyu kocha aliyejijengea heshima kubwa anatuchukulia poa sana Watanzania. Amekuwa akitoa lugha za kejeli kwa wachezaji wa Tanzania bila staha akaachwa, sasa anataka kuhujumu Simba ambayo inawakilisha nchi tena waziwazi si kutuona wadwazi?

Kama taarifa hizi ni kweli huyu kocha atakuwa amepitiliza sasa. Amekosa namna ya kuwasaidia hao AS Vita huku akiheshimu kuwa analipwa mshahara na Watanzania?

Ni vizuri akakanusha taarifa hizi kama si kweli ili zisimchafulie sifa nzuri aliyojijengea hasa namna alivyoijenga Yanga nyakati hizi ngumu kiuchumi kwao.

Kila lakheri chama kubwa Simba, mnawakilisha nchi, lindeni heshima ya taifa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Simba itafungwa kwa sababu za kisaikolojia, hivi Zahera anawahujumu kweli? Hivi AS Vita hawaijui Simba hicho ndio mnachodhani kwamba Zahera anatoa siri zenu. Kwa mpira wa kisasa timu zinafahamiana vizuri tu tena zinafanyiana uchunguzi mapema. Kalieni uchawi mtapigwa mapema.
 
Mimi sijaelewa Zahera ana ihujumu vipi Simba kwa kushiriki kwake na timu ya As Vita. Yule sio mtanzania ni mkongo, na ile As Vita ni timu inayotokea Congo, Kocha wa Vital ni kocha mwenzie anayefundisha nae timu ya taifa ya Congo. Tatizo lipo wapi kwa Zahera kumpa mbinu za kiufundi kocha mwenzie? Hapo hakuna hujuma, labda kama Zahera anafanya namna ili marefa wahongwe, au kama anafanya mbinu chafu zisizoruhusiwa kwenye mpira wa miguu. Lakini kama anaisaidia Vita kwenye mambo ya kiufundi kwenye uchezaji wa mpira basi kwa upande wangu sioni hiyo hujuma kwa timu ya Simba.

Na pia Zahera halipwi mshahara na watanzania, bali analipwa mshahara na timu ya Yanga ambao ndio maasimu wa Simba.
Sent using Jamii Forums mobile app
WACHUKULIE CHANGAMOTO ANAZOWAPA ZAHERA KAMA FURSA WATAFANIKIWA.
 
Zahera yupo Congo,ni kocha msaidizi wa team ya taifa ya Congo. Congo DRC wanacheza na Liberia Alhamisi ijayo. Manara mpumbavu tu,badala ya kufocus kwa team ya Simba yupo busy na whereabouts za Zahera. What for?
Afadhali umewapasha ukwreli wenzako. Good narration!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom