Zahanati ya nchini India, imejitolea kumsaidia mwanamme Mrefu (Baraka Erias) kutoka Tanzania

JaffarMohammed

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
763
279
Zahanati moja nchini India imejitolea kumsaidia mwanamme kutoka nchini Tanzania, ambaye aliambiwa kuwa kutokana na urefu wake, hawezi kufanyiwa upasuaji nchini Tanzania.

Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery, ameiambia BBC kuwa wanaweza kumsaidia Baraka Elias, ambaye madaktari mjini Dar es Salaam wanasema hawezi kutoshea katika kitanda cha hospitali.

Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anasema anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia alipoanguka. Pia aliambiwa kuwa hangeweza kutoshea kwa mashine ya X-ray kutokana na urefu wake.

"Nina uhakika kuwa bwana Elias atapata nafuu hivi karibuni, wakati akifahamu kuwa kuna mtu mbali sana anajaribu kumfanyia maabo kuwa sawa," Dr Shaila Raveendran anayeongoza zahanati ya Speed Recovery nchini India, aliambia BBC.

Bwana Elias anatajwa kuwa mtu mrefu zaidi nchini Tanzania.

Chanzo: BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom