Mukundumbusya
Senior Member
- Aug 11, 2016
- 168
- 142
Nathamini sana na najali sana kazi ngumu na nzito wanazofanya hawa watalaamu wetu wa tiba, tena labda hata kwa mishahara ambayo haiwaridhishi. Lakini ukikubali kufanya kazi inabidi ufanye kwa bidii.
Leo asubuhi ya saa tano nimeingia Zahanati ya MONGOLA NDEGE, cha kwanza kabisa nikasoma bango lao: NI KWAMBA ZAHANATI INAFUNGULIWA SAA 2 ASUBUHI NA KUFUNGWA SAA 11:30 JIONI.
nilipofika ndani nimekuta watu wengi mapokekezi na wengine sehemu zingine na wengi wao wakiwa wana nyuso za kuchoka. Moyoni nikajisemea labda kwa sababu ni wagonjwa.
Baada ya kama dakika tano hivi akaja mama mmoja akiwa na vifaa vya usafi na kuanza kufanya usafi na kusumbua wagonjwa. Swali likanijia akilini kuwa: Je kama zahanati inafunguliwa saa 2 asubuhi, wakufanya usafi inabidi afanye saa ngapi? Kabla ya saa ya kufunguliwa au baada ya kufungua?
Pili baada ya kumaliza heka heka za reception na kukumbana na mareceptionist wa mwendo kasi wakiwa na smartphone in hand wakilike na kucomment kwenye social networks tukaanza kutafutana na vijana wanaojiita madaktari, nao ni mwendo wa haraka. Kuna vyumba 2 nilivyo viona vya madaktari lakini wote hawakuwepo na kusababisha watu kuwa wengi na wengine kukosa sehem za kukaa. Baadae kijana mmoja mrefu mwenye ndevu za kuchonga akiwa na smartphone mkononi akaingia kwa mikogo. Nusu saa nzima akapita bila kuita mgonjwa hata mmoja na badae akaita wawili afu akaondoka na kurudi ka baada ya dakika 20 hivi. Akaendelea kuita na kuita.
Zamu ya mke wngu ikafika akaingia na kadi yake alipotoka nikaichukua na kusoma alicho kiandika, lakini kabla nilimuuliza mbona umetoka mapema, umemweleza vizuri? Akajibu daktari yupo busy na simu. Kuangalia kwenye kadi sentence ya kwanza ni loss of appetite, nkashituka kidogo kwani mpenz wangu kwa kipind hiki ambacho hayuko sawa anakula sana tena mara kwa mara. Ikabidi nimuulize vipi huna hamu ya kula akanijibu hapana.
Hitimisho, jamani madaktari wetu jueni kuwa mnasimamia urekebishaji wa afya za watu kuweni makini na kazi zenu hizo smartphone zitakuwepo hata baada ya kazi.