ZAHANATI HEWA ILALA sh180M zaliwa!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,515
11,834
Wana JF TUCHUKUE HATUA GANI YA HARAKA NA MAKUSUDI?KWA KURA NAONA TUNAJIDANGANYA!KILA SIKU WATU WACHACHE SANA WALIOMADARAKANI WANAKULA JASHO LETU SISI IMEBAKI KUPOST TUU NEWS HUMU NA KUANGALIA UDINI KUMUACHA ADUI UFISADI UKITUMALIZA!soma mwananchi leo au anayeweza a post hiyo news hapa!
 

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,272
4,539
Sh180m zatumika Ilala zatumika zahanati hewa Send to a friend Thursday, 18 November 2010 22:27 0diggsdiggPamela Chilongola HALMASHAURI manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam imeingia katika kashfa nzito ikidaiwa kutumia Sh178,000,000 kwa ajili ya matumizi ya Zahanati ambayo hata hivyo imebainika kuwa ni hewa.Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Ilala umeonyesha kuwa fedha hizo ziliidhinishwa kwa mafungu tofauti kati ya mwaka 2005 hadi Januari 2010 ili zitumike kwa ajili ya Zahanati ya Mogo ambayo hata hivyo haipo kwenye manispaa hiyo wala eneo jingine jijini Dar es Salaam.Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Grace Magembe aliithibitishia Mwananchi kuwa Zahanati hiyo haipo, ingawa kwenye kumbukumbu mbalimbali za matumizi ya halmashauri hiyo kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2010 inaonekana kutengewa fedha ambazo zimetumika.“Mimi siijui na sijawahi kuiona Zahanati ya Mogo," alikana. "Pia sijawahi kutembelea zahanati za Vingunguti na Kipunguni, lakini kama ilivyoonyeshwa, kila mwaka wa fedha zinatolewa Sh 35,600,000 milioni kwa ajili ya kununua vifaa na ujenzi wa Zahanati ya Mogo na Sh19,775,523 milioni kwa ajili ya Zahanati ya Vingunguti Kipunguni,” alisema Magembe.Hata hivyo alitupia mpira huo kwa mchumi wa manispaa ya Ilala akisema ndiye anayeweza kuzungumzia hayo kwa upana zaidi.Mchumi msaidizi wa Manispaa ya Ilala, Musa Lyuti naye alisema kuwa hakuna Zahanati ya Mogo katika Kata ya Kipawa, lakini akasema inawezekana kuwepo kwa jina hilo la Zahanati ya Mogo ni makosa ya uchapishaji kwenye utekelezaji ya halmashauri hiyo.Alisema Zahanati ya Vingunguti Kipunguni ipo katika hatua ya msingi ya awali ipo kwenye mikakati ya kuendelea na ujenzi huo."Mimi ninachojua zahanati ya Mogo haipo isipokuwa inawezekana ni makosa ya uchapishaji ambayo imeonyesha Zahanati ya Mogo, iliyopo Majumba sita inawezekana ni Zahanati ya Mongolandege ya Kata ya Ukonga,” alisema Lyuti.Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alimtupia mzigo mchumi wa Manispaa hiyo akisema kuwa yeye ni mgeni katika manispaa hiyo aliyefika mwaka 2010 hivyo mipango iliyopo aliikuta Source: mwananchi
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
251
Jamani Jamani jamani nini tena hiyo?
Ufisadi ufisadi ufisadi gani tena huo?
Jamani jamani jamani kataeni uchafu huo
Sheria pitisha jamani mafisadi kunyongwa kumo

Jamani jamani jamani wajibu wa nani huo?
ufisadi fatilia ufisadi wakati muafaka huo
jamani tujue jamani nchi yetu yauzwa hiyo
sheria pitisha jamani mafisadi kunyongwa kumo

Mazoea ni kama umimi kugeuka ugojwa huo
ufisadi fatilia ufisadi wa nini tena huo
jamani nchi yaliwa jamani ninani okoa hiyo
sheria pitisha jamani mafisadi kunyongwa kumo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom