Zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura imeiva

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Zabuni ya kuingiza nchini majenereta ya kukodisha kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 260 na kumaliza mgawo, imeiva na inatarajiwa kufunguliwa wakati wowote, kuanzia leo.
Kuingizwa kwa majenereta hayo nchini, ni katika utekelezaji wa mpango wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa kumaliza mgawo unaoendelea kuiathiri hivi sasa mikoa inayopata umeme katika Gridi ya Taifa ifikapo Julai, mwaka huu.
Mikoa pekee, ambayo haipati umeme katika Gridi ya Taifa, ni Kigoma, Mtwara, Lindi, Rukwa na Ruvuma.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Badra Masoud, alisema jana kuwa zabuni hiyo inatarajiwa kufunguliwa wiki hii.
Badra alisema hayo, alipotakiwa na NIPASHE, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana kueleza Tanesco imefikia wapi katika kupata majenereta hayo.
Akijibu swali hilo, alisema kwa ufupi: “Zabuni inafunguliwa wiki hii.”

Alipoulizwa inawezekanaje zabuni hiyo kufunguliwa wiki hii wakati jana ilikuwa Ijumaa, alijibu: “Hadi Jumamosi tunakuwa kazini.”
Alisema kazi ya kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 160 (Dar es Salaam megawati 100 na Mwanza megawati 60), kuanzia mwakani, imekwishaanza na kwamba, wakandarasi wako kwenye eneo husika wakiendelea na kazi hiyo.
Hata hivyo, alisema mgawo wa umeme bado haujasitishwa na kwamba, umeme unaopatikana hivi sasa, unatokana na hali ya maji kutegemea na mvua kwani maji katika Bwawa la Mtera linalotegemewa kwa uzalishaji umeme wa uhakika, hayajatosha kuweza kukidhi mahitaji ya uzalishaji umeme wa uhakika.


Source: Nipashe 18th April


My take:

Hivi Serikali haiweziKununua mitambo yake yenyewe?! Ukosishaji huu wa mitambo si ndiyo unaleta mianya mingine ya ufisadi Richmond nyingine. mambo ya kulipa capacity charge na vipengere vingine vya kijingajinga kwenye mikataba na kuliingiza taifa kwenye matatizo huko mbeleni.
 
JB hili jambo liko wazi kabisa lakini watu wanaona kuwa ukinunua utakuwa umemaliza mradi wa kujiongozea kipato kwa kweli haingii akilini kuacha kununua tunataka kukodisha.
 
Kanchi kadogo(kiuchumi)
Kanchi ka watu wadogo(masikini walio kandamizwa na viongozi mambumbu na waroho)
Kanchi ka kitu kidogo (watawala wamewekwa mifukoni na wajanja)
kanchi kanaitwa Tanzania!
Ndio maana yote hayo....
 
Back
Top Bottom