Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
NI usiku wa manane, mvua inaendelea kunyesha kwa nguvu na upepo katika Jiji la Dar es Salaam wakati huu wa masika, lakini kwa Mohammed Sultan (57), mkazi wa Mbagala Kichemchem, kwake ni majanga.
Anajikuta akigonga katika nyumba mojawapo iliyoko upande wa juu kwa nia ya kupata hifadhi baada ya mafuriko kuikumba nyumba yake iliyo pembezoni kabisa mwa Mto Mzinga na ingawa mvua zilizonyesha hazijawa kikwazo kikubwa kwa wananchi wengi wa Jiji la Dar es Salaam, kwake ni changamoto.
Hayuko peke yake, bali ameongozana na mkewe Salma (34) pamoja na watoto wake 10, sita kati yao wakiwa wamezaliwa na mama tofauti ambapo watatu ni kwa ndoa yake ya kwanza, na watatu kila mmoja ana mama yake, huku umri wao ukiwa chini ya miaka 14 kama ilivyo kwa watoto wengine watatu waliozaliwa na Salma.
“Tumeambiwa tuzae tuijaze nchi, tena hata Mfalme ....
Kwa habari zaidi, soma hapa => http://www.fikrapevu.com/zaa-mpaka-mayai-yaishe-kikwazo-cha-uzazi-wa-mpango-tanzania/