ZA NDANI KABISA: Waamuzi sasa wanafungiwa kimya kimya

Mcanada

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
982
1,904
waaamuzipiic.jpg
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ya kufungiwa kwa waamuzi wawili Amina Kyando na Ahmed Arajiga kwa kipindi cha miezi sita ingawa taarifa zao hazijatangazwa kama ilivyo kawaida.

Habari za ndani kutoka kwenye Kamati ya Waamuzi Nchini, zilieleza kuwa waamuzi hao walifungiwa kutokana na kutozingatia sheria 17 za soka ambapo Aragiga alifanya kosa mechi ya Azam FC na Yanga pamoja na ile ya Prisons na Simba.

Kwa upande wa Amina yeye aliharibu mechi Azam FC dhidi ya Geita Gold na ile ya Namungo na Coastal Union.
Chanzo hizo kilieleza kuwa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu baada ya kupitia matukio ya michezo hiyo ilibaini kuwa wamefanya makosa hivyo kutoa uamuzi huo wa kuwafungia.

Habari za ndani zaidi inasema kuwa kamati hizo mbili hazijatangaza wazi adhabu ya uamuzi huo wa kuwafungia lakini ukweli ni kwamba wamefungiwa kimya kimya.

Mwanaspoti lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nassoro Amdun ili kuelezea juu ya adhabu hiyo na kwanini hawajatangaza alisema kuwa wenye mamlaka ya kutangaza ni Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu.
"Wao wakikutana na kufanya maamuzi yao ndiyo huwaleta kwetu, lakini juu ya hawa wawili hata mimi nimesikia kama nyie tu mlivyosikia, inawezekana ni kweli ama si kweli.

"Kamati hiyo ikisema waamuzi wanarudishwa kwetu, tayari inakuwa imefanya maamuzi yao kama ni kuwafungia, kuwapa adhabu na mambo mengine, wanawaleta kwetu kwasababu sisi ndiyo tunawapangia ratiba, hivyo ni kama kutupa taarifa tu, nadhani watu sahihi wa kutangaza ni hiyo kamati," alisema Amdun.

Chanzo: Mwananchi
 
Mechi ijayo sudani refa ni aragija anachezesha hadi nje ya uwanja
 
Back
Top Bottom