Tetesi: Za ndani kabisa, Biteko kuwa makamu mwenyekiti wa ccm

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,675
55,843
Tetesi za ndani kabisa kutoka viunga vya Kizimkazi zinasema mama anamtaka Biteko kuwa ndiye awe makamu mwenyekiti wa ccm.

Endapo itakuwa kama inavyosemekana, je, nani atachukuwa nafasi ya unaibu waziri mkuu? Au nafasi hii itafultiliwa.mbali??
 
kwani inashindikana kua Naibu waziri mkuu na vile vile ukawa Makamu mwenyekiti wa CCM bara?🐒
 
Sijui itakaaje, maana cheo chenyewe cha unaibu waziri mkuu hakipo kwenye katiba. Kichwa cha Samia ndiyo kinajua majukumu ya cheo hicho.
kwani wizara ya mipango na uchumi iko kwenye katiba?🐒
 
Tetesi za ndani kabisa kutoka viunga vya Kizimkazi zinasema mama anamtaka Biteko kuwa ndiye awe makamu mwenyekiti wa ccm.

Endapo itakuwa kama inavyosemekana, je, nani atachukuwa nafasi ya unaibu waziri mkuu? Au nafasi hii itafultiliwa.mbali??
Awe tu yeyote yule. Ila, habari za fomu moja ya urais hatutaki. Kila mtu ajipime ubavu hakuna mambo ya kudra
 
Kwa hiyo move nadhani ndio anaandaliwa kuwa makam wa Raid 2025,ni calculated movement,japo sijui kauli ya yule mkuu wa majeshi , General mkunda kama inamhusu huyu jamaa!!

Je Bashungwa atakomesha Teka Teka!!?au kawekwa pale kuwapoza TEC coz jamaa ni kipenzi wa harambee za kanisa namaaskofu!!

Na hiyo move ya kumchafua kinana kupitia huyo Binti imekaaje!!?he ni kweli Born towns wamefyata Kwa kizmkazi!!?

He kizimkazi ana Baraka zote za deep state kwamba by 2025 no yeye !?japo amekiuka maagizo Yao Mengi!!?ikiwemo agizo la Uchaguzi serikali za mitaa usubiri katiba mpya ambayo ilishapaswa kuwa imeanza kuandikwa Hadi wakati huu!!?

He Ile operation Yao ambayo hao deep state waliiahirisha na Sasa wameirejesha yaani "original plan in and out,itafanikiwa yaani code PJLK!!?

Bado mapema Sana ngoia tuone kazi!!
 
Ngoja tusubiri Lucas Mwashambwa aje atuthibitishie. Nyie makamanda, aka nyumbu, hamuaminiki. Mnaweza kutulisha matangopori.
 
Naibu wa cheo kilichopo kwenye katiba (waziri mkuu). How?

Hapa ni sawa na kuwa mchungaji .kuwa msaidizi wa shekhe. How?
kwani imeathiri wapi hiyo katiba? Na he, huyo kijana ni wa kwanza kua Naibu waziri mkuu au ni gubu tu 🐒
 
Awe tu yeyote yule. Ila, habari za fomu moja ya urais hatutaki. Kila mtu ajipime ubavu hakuna mambo ya kudra
Fomu moja ndiyo tumaini la mwisho lililobakia kwa mkizimkazi kuendelea kuwa pale Magogonj. Likibatilishwa hili atavua ushungi na atatembea kwa mguu kurudi kwao.
 
kwani imeathiri wapi hiyo katiba? Na he, huyo kijana ni wa kwanza kua Naibu waziri mkuu au ni gubu tu 🐒
Haijalishi ni wa pili au ni WA mia moja. Ishu ni majukumu ya kikatiba atayagusa vipi wakati katiba haimtambui?

Usifurahie ubakwaji wa katiba, kuna siku utajutia madhara yake yakikufikia.
 
Back
Top Bottom