Za mchawi 40 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Za mchawi 40

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jan 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td align="left" bgcolor="#cccccc"><table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td class="news1"> ZA MCHAWI 40

  </td> <td class="news1" align="right" width="150">uwazi</td> </tr> </tbody></table></td> </tr> <tr> <td bgcolor="#999999">[​IMG]</td> </tr> <tr> <td class="morenews" align="left" bgcolor="#f3f3f3" valign="top">
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->​

  Tukio hilo lililoshangaza wengi, lilijiri Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, Jumatatu iliyopita majira ya asubuhi ambapo wakazi mbalimbali wa eneo hilo walikuwa wakielekea kwenye majukumu yao ya kila siku.

  Mtu huyo ambaye baadaye ilithibitika kuwa ni mchawi kutoka kwa watu waliomfahamu, ilidaiwa kuwa, alipiga mwereka eneo la nyumba hiyo ambayo ni mzee mmoja mganga wa kienyeji.

  Habari zinadai kuwa, mwanga huyo alikuwa katika safari zake za kila siku za kuwanga angani na baadaye kurejea nyumbani kwake kumalizia usingizi, lakini akiwa hajui kama eneo alilokuwa ‘akivinjari’ usiku huo, kwa chini lilitegwa ‘bunduki’ yenye risasi na mganga huyo hivyo kujikuta akitunguliwa na kuangukia nje ya nyumba hiyo.

  Akiongea na Mwandishi Wetu, mmoja wa watu walioshuhudia mtu huyo akiwa nje ya nyumba hiyo kama alivyozaliwa alisema kuwa, walimkuta mwanaume huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 65, katika kibaraza cha nyumba hiyo majira ya saa 12 asubuhi huku akionekana kuweweseka kwa kusema maneno yasiyojulikana.

  “Mimi na mwenzangu tulikuwa tunaelekea kazini asuhuhi kama saa kumi na mbili hivi, ghafla tulishtuka tulipomuona huyu mzee akiwa amelala katika kibaraza cha nyumba hii, tulichofanya tuliwaamsha wenye nyumba,” alisema shuhuda huyo.

  Aidha, muanika habari hiyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuwaamsha wenye nyumba, walitoka nje kushuhudia ambapo pia majirani wengine walifika kumshuhudia mzee huyo ambaye alikuwa uchi wa mnyama.

  Aliendelea kusema kuwa, mwenye nyumba hiyo ambaye ni mganga wa kienyeji aliwaambiwa watu waliofurika eneo la tukio kuwa, mtu huyo alianguka usiku baada ya kumtungua kwa risasi zake ambazo huzitega ili kumlinda na wanga kama huyo.

  Alisema kuwa, mtu huyo alikuwa na nia ya kuwanga katika nyumba hiyo lakini alizidiwa na mashambulizi ya mganga huyo wa kienyeji ambaye alitamba kuwa, yeye ni moto wa kuotea mbali.

  Hata hivyo, mganga huyo alisema kuwa, yeye si kama waganga matapeli wanaopanga dili za kunasa wachawi wakati si kweli, bali yeye ni mganga wa kweli na ndiyo maana alikuwa ndani akiendelea kuuchapa usingizi na familia yake wakati mwanga huyo anatunguliwa na wapita njia kumwona asubuhi.

  “Sijisifu, lakini mimi si wale waganga matapeli, wanasema mchawi kanaswa, kumbe si kweli, tena simu wanapiga wenyewe kuita askari, mimi nilitegesha risasi zangu, jamaa kazikaribia zimemfyatukia,” alisema mganga huyo.

  Ilielezwa kuwa, pamoja na mtu huyo kunaswa na tunguri zake, lakini alikataa kata kata kutaja jina lake wala alikotokea achilia mbali alikokuwa anakwenda.

  Hii si mata ya kwanza kwa watu kukutwa uchi nje ya nyumba za watu ikidaiwa kuwa, wanaanguka kutoka angani walikokuwa wakiwanga au kufanya vitendo vya kishirikina.

  Serikali na imani mbalimbali za dini zimekuwa zikilaani vitendo vya kishirikina hasa kutokana na ukweli kwamba, vimekuwa vikisababisha mitafaruku mbalimbali katika jamii.

  Hivi karibuni pia, mwanamke mmoja, mkazi wa Mbagala Kizuiani, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, alidaiwa kukutwa akiwanga nje ya nyumba ya mganga mmoja wa kienyeji maeneo ya Tabata, jijini Dar.

  Hata hivyo, baadaye ilikuja kubainika kuwa, mwanamke huyo hakuwa mchawi, bali ulikuwa ni mchezo uliochezwa na mganga mmoja kwa lengo la kujikuzia jina na kupata wateja wengi kwa kuaminika ana dawa za kweli.


  http://www.globalpublisherstz.com/index.php?newsid=5991
  </td></tr></tbody></table>
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umasikini tu unatesa watu hawa...Wanatafuta senti za uji wa jioni. Poor them!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,341
  Trophy Points: 280
  Wachawi wadumu milele yote
   
 4. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ???????? :confused::confused::confused::confused::confused::confused:
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  teh teh teh sangoma huyooo....kashikwa...
   
 6. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa alisaidiwaje kurejea angani aendelee na safari yake ?? Au aliendelea kukaa utupu na nyeti zake zote hadharani !!!!!!!!! Looh, salaaaleeeeeee.
   
 7. m

  mjukuu2009 Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  bora mchawi kuliko fisadi.
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mpelekeni huko Salva Rweyemamu aliyekubaliana na utabiri wa Yahya Hussein!!! Yaani such low acceptance and belief!!!
   
Loading...