Yvonne Chakachaka atimuliwa Uganda kwa kufanya shughuli ya kujiingizia kipato bila kibali cha kazi, Mwenyewe akanusha na kuahidi kurejea Uganda

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,982
9,873
Uganda deports Yvonne Chaka Chaka for lack of work visa

"The ordinary visa cannot enable her to perform in any income-generating activity within the country.

This has been done by immigration officials and the security team to help maintain the integrity of our immigration rules."

=====
1578479803620.png
Mamlaka nchini Uganda zaelezwa kumuondoa Uganda Mwanamziki Yvonne Chaka Chaka kutoka Afrika Kusini ambaye alitarajiwa kutumbuiza katika tamasha la usiku wa mwaka mpya Ikulu ya Mengo huko Kampala.

Taarifa zinaeleza kuwa msanii huyo aliondolewa Uganda kutokana na kukosa Visa inayomruhusu kufanya kazi nchini Uganda.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda Bwana Bwana Fred Enanga alithibitisha kwamba msanii huyo aliondolewa Uganda kutokana na kutokuwa na Visa inayomruhusu kufanya kazi nchini Uganda.

Alisema kuwa "Nautaarifu umma kuwa Maafisa wa uhamiaji wamemuondoa Bi Mhinga Yvonne, maarufu kwa jina la Yvonne Chaka Chaka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, ambapo alipanda ndege yake ya pili kurejea Afrika Kusini".

Aidha, Bwana Enanga alifafanua kuwa hapo awali Chaka chaka alikuwa na Visa ya kawaida ambayo baadaye ilifutwa na Maafisa wa Uhamiaji baada ya kugundulika kuwa alikuwa amekuja kikazi (kutumbuiza) msanii katika moja ya hafla ya Mwaka Mpya.

Kwa upande mwingine,Inasemekana kuwa Yvonne Chaka Chaka wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Uganda alisikika akimsifu Bobi Wine na akamtaja kama Mandela mpya.

Yvonne Chaka Chaka akanusha, asema atarejea kutumbuiza Uganda:
Kufuatia madai hayo Yvone Chaka Chaka akana kufukuzwa Uganda na asisitiza kuwa kwake Uganda ni kama nyumbani kwake na siku moja atarejea kutumbiza.

Aidha, Chaka Chaka amefafanua kuwa hakufanikiwa kuonekana katika Tamasha hilo usiku ule kutokana kutokuelewa mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea katika tamasha hilo na alikosa ufafanuzi kwa wahusika.

" sijafukuzwa, sijakamatwa. Kila kitu ni sawa. Najua watu wangu wana wasiwasi, nchi yangu ina wasiwasi, mume wangu ana wasiwasi .... lakini niko sawa. '' Chaka Chaka alisema

Baadhi ya Tweets alizozituma Chaka Chaka kukana madai ya kufukuzwa
1578481257425.png


1578481440036.png
 
Naipongeza Sana immigration department ya Uganda. Hakuna kupindisha taratibu eti kwa vile Ni msanii. Katika nchi zao wenzetu wanafanya hivyo hivyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom