Yuwapi Mh Zitto?

GY

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,279
126
Jamani wakuu, yukwapi Mh Zitto Kabwe, sijamsikia muda kidogo humu ndani na nina hamu kweli ya kuzungumza nae suala la Nyumba mbili kwa bilioni mbili unusu
 
Mh. Zitto kabariki maamuzi

Ndio sababu ya kukimbia jukwaa hili sikuizi nini baada ya kuwa na mengi ya kutakiwa kujibu. Huyu dogo sijui keshanunuliwa kama Ronaldo alivonunuliwa na madrid
 
mnamtaka wa nin?
tunaomba tupumzike kidogo na habari za huyu kijana,EBO!
jaribu kukonsetreti kwenye muungano na MPASUKO WAKE
 
mnamtaka wa nin?
tunaomba tupumzike kidogo na habari za huyu kijana,EBO!
jaribu kukonsetreti kwenye muungano na MPASUKO WAKE

Hapana hatumtaki kwa ajili ya mambo yake, tunamtaka kwa ajili ya kuzungumza nae kama mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mashirika ya umma, atuambie hili la nyumba za vigogo wa BOT likoje mbona anaonekana amepoa sana kwenye hilo?
 
Zitto kaisha isha.
 
Hivi nini msichoelewa kuhusu siasa za AFRICA? siasa za Africa na zifananisha sana na dini mpya zinazoibuka kwa ajili ya maslahi ya mchungaji na sio kwa maslahi ya kiroho ya waumini.
 
Hivi nini msichoelewa kuhusu siasa za AFRICA? siasa za Africa na zifananisha sana na dini mpya zinazoibuka kwa ajili ya maslahi ya mchungaji na sio kwa maslahi ya kiroho ya waumini.

Hata yeye alikuwa anazisema sana siasa za Africa, tukajua yeye si mmoja wao. Heh kuja kutahamaki, mwenzetu hatumuoni.

Jamani popote ulipo ndugu yetu Zitto Zuberi kabwe tafadhali fika JamiiForums jukwaa la siasa kuna ndugu zako wanakutafuta!
 
tupumzishe na habari za huyo zitttooo please tuconcentreate na ujenzi wa taifa letu changa,achana na habari za individual cheap popularity
 
Kakaa kimya kuhusu Gavana maana ushahidi wa shiria ya manunuzi ya umma ulionyeshwa kufuatwa hatua kwa hatua. Zitto yeye ni msomi na hivyo sii mtu wa kupinga tu kila kitu hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo. Serikali nayo imehamua kwa gharama yoyote kumtetea Ndulu hata kwa ushahidi wa kutengeneza, maana wameona wakiachilia hili litakuwa mbaya zaidi ya lile la EPA. Pia ukizimgatia ndulu alikuwa naibu wa balali na kama wakimwachia huyu tena wataharibu kabisa mchongo. Serikali ya JK kwa sasa inakaba hata penalty.
 
Ndio maana tunamuita aje ayaseme hayo unayoyasema wewe. Na hilo ndio tatizo letu, focus yetu hua ni kwenye kutazama kama taratibu za tenda na malipo zilifuatwa basi. Hatuendi zaidi ya hapo.

Hoja ya msingi hapa ni kwanini chombo kinachosimamia uchumi dhaifu wa nchi masikini kama hii kiwe ndo kinara wa kutumia pesa kama vile kinasimamia giant economies kama za Marekani na Ulaya? Unakumbuka gharama za majengo ya ofisi zao. Kwa sh bilioni 360 ungeweza kufanya mambo mangapi kwa nchi masikini kama hii. Bush na MCC yake walituletea takriban bilioni 900 ambazo wanazitoa kwa miaka mitano. impact ya msaada kama huo ni hadithi nyingine ya kusimulia. Hizi za majengo ya benki kuu ni zaidi ya theluthi moja ya hizo za msaada wa marekani.

Kamati ya bunge sio auditors wa kuchunguza tu kama tender process na financial regulations nyingine zilifuatwa, wao wanapaswa kutazama hili ninalolisema.

sasa usomi huu wa wanasiasa na watendaji wa serikali wewe unaupimaje?
 
tupumzishe na habari za huyo zitttooo please tuconcentreate na ujenzi wa taifa letu changa,achana na habari za individual cheap popularity

Mkuu simzungumzii mtu, nazungumzia nafasi yake kuhusiana na suala la nyumba za BOT

mmechoka nini sasa, na ni nchi gani hiyo mnayoijenga. Hapa inajengwa nchi au yanajengwa mahekalu?
 
Back
Top Bottom