Yusuph Manji kwa haya matatu naomba niwe Mganga wako nyota irudie kung'aa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,363
108,402
Kwa haya mambo matatu ( 3 ) ni ishara tosha kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuph Mehboob Manji siku zake za kuelekea katika ' umasikini ' mkubwa sana na kuja kuumbuka mno huko mbele sasa ' zinahesabika ' hivyo naomba tu ' nijitolee ' kwa muda kuwa ' Mganga ' wake ili niweze kumpa ' mizizi ' yangu fulani ambayo itaweza kurudisha ' nyota ' yake ya kutopendwa, kutoaminiwa na kukataliwa katika kila ' analolijaribu ' nchini Tanzania hadi kupelekea kuonekana ni ' Fisadi ' Kuu na mambo yake yaweze kuwa mazuri.

Lakini katika hizo ' ndumba ' ambazo nitampa hazitaishia tu kumfaidisha yeye Manji kama Yeye ila zitaweza pia kuisadia hadi na Klabu yake ( ambayo na Mimi pia naishabikia ) anayoiongoza ya ' Chura Churani ' ya Yanga ili na yenyewe izidi kung'aa na kufanya vizuri.

Mambo yenyewe ni:

  1. Kukataliwa kununua ' Ufukwe ' wa Coco Beach.
  2. Kukataliwa kuimiliki Klabu ya Yanga huku wenye Klabu wakimvizia kumchapa ' bakora '.
  3. Kufukuzwa katika Jengo la Quality Plaza kwa kushindwa kulipa ' Kodi ' anayodaiwa.
HOFU.

Kama hali hii Manji hatoiangalia kwa ' umakini ' mkubwa na kunitafuta Mimi nimsaidie ' Kimazingara ' nawaona hawa Wachezaji akina Kamusoko, Ngoma, Niyonzima, Mbuyu, Bossou, Chirwa, Tambwe na huyu ' mgeni ' Zulu wakianza kushindia mihogo ya kukaanga, tembele na kushindia maji ya ' Kandoro ' pale mitaa ya Twiga na Jangwani.

Masikini Yusuph Manji pole sana.......
 
Badala ya kuhangaikia ndugu zako wanaoshinda njaa na kung'atwa na kunguni usiku,unashabikia mambo usiyoyajua
 
Acha,kumwombea na kumwazia vibaya binadamu mwenzo.we hapo ulipo una nin? Iyo miziz si ikusaidie wew kwanza.
 
"Masikini (tena mwenye ngozi nyeusi) anapoonyesha uhitaji wa kumsaidia Tajiri (mwenye ngozi nyeupe)."

sijui tumerogwa nini watu wenye ngozi nyeusi....?
 
Back
Top Bottom