Yusuph Manji achukua fomu za kugombea uenyekiti wa Yanga!

Embu muulize Rage alifuata nini magereza na sasa hivi yuko wapi anaongoza chama gani na timu gani?Ukijibu haya utanyamaza.
Huwezi kunieleza lolote Mkuu. Fisadi ni fisadi tu na wewe inaelekea ni mmojawao. Mtu yeyote aliyeshiriki wizi wa hela za watanzania na leo hii anajidai eti anasaidia team wapi na wapi. Atoke hadharani aeleze hela za Kagoda period. Wewe ndo wale ambao mnampinga Masaburi. Mbona action imechukuliwa, yuko wapi Simba na UDA yake? Ninajua ninachoongea ndugu ID Anselm!!
 
Hii imekaaje, mbona katibu wa kamati ya uchaguzi wa Yanga Bw. Kaswahili anasema ni mtu mmoja tu aliyechukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya uenyekiti naye ni John Jambele. Ufafanuzi please kwa wana wa Yanga.
 
Manji wana Yanga tunakuunga na kusupport kwa sababu wewe ni mtu muhimu sana kwa maendeleo ya Yanga.Kuna wanafiki wengi wamejaa humu ndani kwa hiyo ukiona comment zao wala usiotetereke wengi wao ni wafuasi wa Rage mzee wa reception kudadeki zao
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo,kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari nimechukua form na nitagombea uenyekiti,kwahiyo naombeni sana ushirikiano wenu ili kwa pamoja tuweze kuipeleka yanga mbele,mungu ibariki tanzania,mungu ibariki yanga!
 
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo,kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari nimechukua form na nitagombea uenyekiti,kwahiyo naombeni sana ushirikiano wenu ili kwa pamoja tuweze kuipeleka yanga mbele,mungu ibariki tanzania,mungu ibariki yanya!

Ha ha ha ha ha
 
Hii imekaaje, mbona katibu wa kamati ya uchaguzi wa Yanga Bw. Kaswahili anasema ni mtu mmoja tu aliyechukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya uenyekiti naye ni John Jambele. Ufafanuzi please kwa wana wa Yanga.

Ni vimuhemuhe tu vya mashabiki wenzio,kuona Manji kaenda kuchukua Form jana bila kutafuta ukweli kuwa Form chukuliwa ni za kina nani tayari mashabiki wenzio matumbo joto,....unajua mimi nilikuwa sijui kuwa mashabiki wa Simba wanamwogopa Manji namna.
 
Jamani mbona Simba mlikuwa na Azim dewji,na sasa mna Husbands of Simba (friends of simba) na hatuwapigii makele?
 
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo,kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari nimechukua form na nitagombea uenyekiti,kwahiyo naombeni sana ushirikiano wenu ili kwa pamoja tuweze kuipeleka yanga mbele,mungu ibariki tanzania,mungu ibariki yanga!
kati ya siku ambazo zimenichekesha, leo moja wapo, kumbwe huyu spika ndo manji? ati we manji,....haya bwana, karibu yanga, pengine hizo hela wanazosema umefisadi nitazifaidi kupitia timu yangu ya yanga labda ipigwe promo iendelee....kwasababu usipofanya hivyo sitafaidi kabisa pesa yako hiyo uliyotuibia watz....hivi ule ugomvi wenu na mengi alokuambia wewe ni fisadi papa umeishia wapi?...halafu nakupongeza kwa kunyamaza kimyaaa baada ya kuambiwa unawaibia uwanja waislam ule wa chang'ombe, walikulalamikia wewe tu wakati kuna jengo la yemen pale ambalo wamenyamaza tu....nasikia walikuomba mil. 150 rushwa ukachomoa....aisee we mkariiii.
 
sisi mashabiki wateule wa simba tunaomba mmuhakikishie huyo manji usalama wake endapo tutawafunga,manake historia inanyesha mkifungwa na cc tu migogoro inaanza,je mtamlindaaa?
 
kati ya siku ambazo zimenichekesha, leo moja wapo, kumbwe huyu spika ndo manji? ati we manji,....haya bwana, karibu yanga, pengine hizo hela wanazosema umefisadi nitazifaidi kupitia timu yangu ya yanga labda ipigwe promo iendelee....kwasababu usipofanya hivyo sitafaidi kabisa pesa yako hiyo uliyotuibia watz....hivi ule ugomvi wenu na mengi alokuambia wewe ni fisadi papa umeishia wapi?...halafu nakupongeza kwa kunyamaza kimyaaa baada ya kuambiwa unawaibia uwanja waislam ule wa chang'ombe, walikulalamikia wewe tu wakati kuna jengo la yemen pale ambalo wamenyamaza tu....nasikia walikuomba mil. 150 rushwa ukachomoa....aisee we mkariiii.
Inshu ya bwana mengi tulishaimaliza long time ago,by the way pls let us discus about yanga africa,itapendeza kama utaniuliza nini malengo yako utakapopata nafasi ya kuiongoza yanga?ingawa nafikilia kujiondoa ktk kinyang'anyiro!







,
 
Mi ni mshabiki wa yanga na si yanga mamluki, binafsi naona matatizo mengi ya uongozi wa yanga uliopita unasababishwa na Manji. Kwani kwenye mpira kuna nini mbona anang'ang;ania sana? Kwa nini aisbaki kuwa mfadhili na awaache watu waongeze? What is so special?
 
[h=3]KWANINI MANJI ANAUTAKA UONGOZI WA YANGA?[/h]

*NI KWELI ANATAKA KUIMILIKI YANGA?

*NA KAMA AKIFANIKIWA KUWA MMILIKI ATAIFANYIA NINI YANGA?

*KWANINI BAADHI YA WANACHAMA HAWAMTAKI?



Kwa kipindi kirefu sasa tangu mfanyabiashara maarufu Bwana Manji ajiingize katika kuifadhili klabu ya Dar Young Africans kumekuwepo na mgawanyiko mkubwa wa kifikra miongoni mwa wanamichezo, wanachama na wapenzi wa Yanga, juu ya madhumuni hasa kabisa ya mfanyabiashara huyo kuisadia Yanga.


Huku baadhi ya watu wakisema Manji ana nia ya dhati kabisa ya kuisadia Yanga na kuifanya kuwa klabu ya kisasa kabisa,huku wengine wakibaki kusema kwamba mmiliki huyo wa Quality Group of Companies anataka kuitumia Yanga kibiashara na kujinufaisha binafsi kwa kutumia brand ya Yanga.


Katika kipindi cha awamu mbili za uongozi tofauti pale Yanga, kuanzia kwa Wakili Iman Madega mpaka uongozi huu uliopinduliwa wa mwanasheria Lloyd Nchunga, Yusuph Manji amekuwa akitajwa kuhusika na migogoro mikubwa iliyojitokeza ndani ya klabu hiyo.


Hivi karibuni baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga hasa wakiongozwa na wazee wa klabu hiyo, waliongoza mapinduzi ya kuuondoa uongozi halali wa bwana Lloyd Nchunga, ambaye mara ya kwanza alijaribu kutuna lakini mwishowe akaachia ngazi mwenyewe baada ya kuandamwa sana kiasi cha kuanza kupokea vitisho na kufanyiwa vurugu. Wazee wakachukua timu huku wakitamba wana zaidi ya millioni 750 za kufanya usajili, lakini TFF ikairudisha timu chini ya uongozi wa katibu mkuu Celestine Mwesiga huku wakiagiza ufanyike uchaguzi kama katiba ya klabu inavyosema.


Uchaguzi ukaitishwa kwa mujibu wa kanuni, na kamati ya uchaguzi ikaanza kutoa fomu za nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga.



Katika hali ya kushtusha siku ya jumatatu mfanyabiashara na mdhamini wa klabu hiyo, Manji akachukua fomu ya kugombea uenyekiti wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya jangwani,huku akimchukulia mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili Abdallah Ahmed Bin Kleb fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji, na hatimaye leo Manji alikuwa mmoja ya wanachama 29 wa Yanga waliorudisha fomu za kugombea nafasi za uongozi mbalimbali ndani ya Yanga.


Kitendo cha Manji kuutaka ubosi wa klabu ya Yanga umeibua hofu na maswali mengi juu ya nia hasa ya mfanyabiashara huyo dhidi ya Yanga, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao siku zote wamekuwa wakimpinga Manji kwa namna moja au nyingine wakidai hana nia nzuri ya klabu yao, wameongea exclusively na shaffihdauda.com na kutoa hoja nyingi sana zinazojaribu kuelezea kwanini hawana imani na mpango wa Manji kuwa mwenyekiti wa klabu yao.


1:MANJI VS IMANI MADEGA NA LLOYD NCHUNGA

Wakati wakili Iman Madega anataka kuingia Yanga alikuwa akipigwa tafu kubwa sana na bwana Manji mpaka akafanikiwa kuutwa uongozi wa klabu hiyo. Lakini baada ya muda kupita kukatokea kutokuelewana baina ya watu hao wawili. Hii ilikuwa ni baada ya Manji kuleta wazo la kutaka Yanga iendeshwe na kampuni. Kwa maana ingeanzishwa kampuni ambayo ingenunua asilimia 51 za Yanga, na asilimia 49 zinazobakia zingekuwa zinamilikiwa na wanachama ambao wangekopeshwa kiasi cha billioni 3 na Manji kwa mkopo wa mwaka mmoja tu, huku akiwawekea sharti kwamba kama wangeshinda kuzilipa billioni 3 zake alizowakopesha ndani ya kipindi walichokubaliana kulipwa na mkopo huo , basi Manji ndio angekuwa mtu wa kwanza kuuziwa hisa zile zile ambazo walishindwa kuzilipia.
Pia katika zile hisa asilimia 51, hakukuwa na sheria zozote za kumkataza mtu yoyote kununua hisa hizo, uwe mwanachama au la ungeweza kununua hisa, hata Manji mwenyewe kama angejisikia kufanya hivyo pia alikuwa na uhuru wa kununua.
Baada ya kuupitia vizuri mpango huo Iman Madega hakuweza kukubaliana na mpango huo kwa hofu, kwamba ule ni mpango ambayo ungeidhuru Yanga.


Baada ya kumshindwa Madega ambaye alifanikiwa kumaliza kipindi chake cha Uongozi, klabu hiyo ikafanya uchaguzi na kupata uongozi mpya chini ya Lloyd Nchunga ambaye naye alipoletewa mpango wa kuanzishwa kwa kampuni na Manji akakataa na matokeo yake timu ikahujumiwa kitu kilichopelekea migomo ya wachezaji, na hivyo timu kufanya vibaya kwenye ligi. Inasemekana baada ya Nchunga kuvimba na kukataa kujiuzulu baada ya kipigo cha 5-0 kutoka watani wao Simba, ndipo bosi Manji alipoanza kutoa mkwanja kwa baadhi ya viongozi na kuwaambia wajiuzulu huku akiwatumia wazee kumtia mshikemshike Nchunga ambaye mwishowe akaamua kujiuzulu na kupelekea kuitishwa kwa uchaguzi mpya.



KIVIPI?

Kiuhalisia tu shilingi billioni 3 ni fedha nyingi sana kwa wanachama wa kawaida wa Yanga ambao ndio wapo wengi kuweza kumudu kuzilipa ndani ya kipindi mwaka mmoja. Hata kama wangemudu kuzilipa basi isingekuwa rahisi unless kuwe kuna mkono wa mtu nyuma yao, na kama wangeumudu kwa uwezo wao basi ni wachache sana wangeweza kufanya hivyo, hivyo mwisho wa siku hisa nyingi sana zingerudi mikononi mwa Manji.
Huku pia kwenye asilimia 51 za kampuni Manji alikuwa na uhuru wa kununua hisa, hivyo kama Manji akazipata labda asilimia 40 ya hisa alizowalipia wanachama kwa mkopo na wakashindwa kuzilipa na huku kwenye kampuni akanunua japo asilimia 15 tu, kwa maana hiyo angekuwa ndio majority shareholder hivyo kumfanya kuwa mmiliki wa Yanga SC.


2: KWANINI HAWATAKI MANJI AIMILIKI YANGA?
Anti-Manji wanasema hawana imani kabisa na Manji kwamba anaitaka Yanga ili kuisadia iwe klabu na yenye mafanikio, bali ni kwa maslahi yake binafsi.
Kwanza wanajenga hoja kwamba Manji hakuingia Yanga kwa mapenzi binafsi bali alisukumwa na sababu za kisiasa kwa kuifanya klabu hiyo inayosadikika kuwa na wapenzi wengi zaidi nchini kuwa kichaka cha kujifunikia madhambi yake baada ya kukumbwa na kashfa ya EPA.
Wanasema Manji tofauti na wadhamini wengine waliowahi kuidhamini na kuisadia Yanga kama akina Gulamali na Mohamed Vilani, ambao walikuwa wakitoa fedha nyingi kuisadia timu yao bila kuidai chochote, lakini Yusuf Manji siku zote amekuwa akiwasainisha kwenye vitabu vya kumbukumbu viongozi kwa niaba ya Yanga kila anapotoa fedha labda ya usajili au kuisadia pale timu inapokwama kiuchumi, na hilo limeshathibitishwa na Manji mwenyewe pale alipokaririwa mara kadhaa akisema anaidai Yanga fedha nyingi bila kuweka wazi ni kiasi gani. Kwa hiyo hawajui ni lini atawadai fedha anazoidai klabu hiyo na kama watashindwa kulipa je atafanya nini?


Anti-Manji wanaendelea kujenga hoja zao kwa kusema kuwa wanahisi kwamba Manji ambaye pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki majengo mengi ya kibiashara hapa nchini anachokihitaji kutoka Yanga kwanza ni kujilipa fedha zote alizotumia kuisaidia klabu hiyo pamoja na zile ambazo zipo nje ya vitabu alizotumia kupata wafuasi waliochini ya himaya yake ndani ya klabu hiyo.


Wanasema wasiwasi wao ni kwamba ikiwa Manji atakuwa mmiliki wa Yanga, ataitumia brand ya klabu hiyo pamoja na assets zake ili kujilimbikizia fedha nyingi kwa kipindi labda cha miaka 3 mpaka mitano na baadae ataliuza tu jina la Yanga ikiwemo timu, na yeye kubaki na assets za Yanga yakiwemo majengo mawili ambayo yote yapo kwenye eneo la kibiashara la kariakoo pamoja na eneo kubwa wanalolimiliki Yanga la Jangwani makao makuu ambapo imegundulika Yanga inahodhi eneo kubwa sana ambalo kwa sasa limevamiwa na baadhi ya majirani wanaoishi karibu na makao makuu ya Yanga-Jangwani.


Endapo Manji ataliuza jina la Yanga na kubaki na assets za klabu hiyo kisha kuzitumia kwa matumizi mengine, klabu hiyo itapoteza sehemu ya historia yake kubwa iliyojijengea.




3: ANTI-MANJI WALIVYOPOKEA TAARIFA ZA MANJI KURUDISHA FOMU BILA TEGEMEO LAO IDD KIPINGU KUSHINDWA KUCHUKUA FOMU.


Baada ya Manji kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa Yanga, kundi la wanachama wanaompinga Manji kwa sababu zao waliamua kutafuta njia za kuweza kupambana nae. Inasemekana wakajaribu kumtumia mtoto wa kigogo wa nchi ambaye nae ana nguvu na ufuasi mkubwa ndani ya klabu hiyo, ili aweze kumshawishi Kanali Iddi Kipingu agombee nafasi hiyo, lakini baada ya Kipingu kushindwa kuhakikishiwa kupewa sapoti ya asilimia 100 ya kuweza kupambana na tajiri Manji akaona bora asijiingize kwenye vita mabayo itaweza kumshushia heshima yake kubwa aliyojijengea kwenye tasnia ya michezo nchini kwa kuangushwa vibaya na Sheikh Mansour wa Tanzania.

NB: HUU SIO MTAZAMO WANGU BALI NI MTAZAMO WA WANACHAMA WA YANGA WANAOMPINGA MANJI. NIMEWASILISHA. BY SHAFFIH DAUDA.

source:
Shaffih Dauda in Sports.

wadau wa yanga angalieni mawazo ya wenzenu hapo ili mchanganue vizuri mustakabali wa klabu yenu chini ya fisadi wenu huyu( kwa mujibu wa Mzee Reginald Mengi ambaye pia ni mwanayanga mwenzenu.....

The Magnificient!!
 
Embu muulize Rage alifuata nini magereza na sasa hivi yuko wapi anaongoza chama gani na timu gani?Ukijibu haya utanyamaza.

Kwa hiyo unataka kuniambia ni mafisadi wanatambiana? Kama ni hivyo ni nani amewapa hiyo nguvu kubwa hivyo kama si hicho chama chenu cha mafisadi kinakumbatia mafisadi kwa kuwa wanawapa michango? Si kwamba namtetea Rage ni kwamba wote Rage na Manji si Watanzania!!!! Si wazalendo!!! Wasomali na Manjis!!! Kwa hiyo hawana uchungu nasi, wao ni maslahi mbele, maslahi yao. Katika post zangu zote hapo hakuna niliyounga mkono uwepo wa Rage Simba, hata moja hakuna kwa kuwa najua wote ni mafisadi, but Manji ni fisadi papa wakati yule Rage ni Fisadi Dagaa!! You get my point Mznga!!
 
Back
Top Bottom