kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 118
- 237
Wakati serikali ya awamu ya sit chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu ikianza kuchukua hatua kutokana na mapungufu yaliyoainishwa katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)watu mbalimbali wametoa mitazamo yao ikiwemo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba anasema Rais Samia Suluhu asifundishwe kufanya kazi aachwe kwani tayari hatua alizochukua ni sahihi.
Ni vyema kumpa nafasi mkuu wa nchi afanye kazi, kwa kuwa hadi sasa kila mmoja ameona na kusikia kuhusu uwezo wake katika utendaji wa juu kwa namna anavyoisimamia serikali na nchi kwa utashi, usikivu na kuwa na uamuzi wenye tija kwa maslahi ya Taifa.
"Tusimfundishe namna ya kufanya kazi hatumtendei haki....niulize kwa haya yanayoendelea je kuna mwenye mashaka tena na uwezo wake hadi sasa? Rais Samia kwetu watanzania ni kiongozi bora anatosha na kwa CCM tunaamini ndicho chama bora, wakae watulie sasa.
"Muhimu tumuombee kwa kuwa ni kiongozi makini anayeamua mambo kwa busara, msikivu na anajua hapa niseme nini, nifanye nini, angeamua kukaa kimya kwa hii ripori kufanywaa kwa kificho tusingejua, lakini kutokana na uchungu alionao kwa nchi akiwa kiongozi anayejiamini ameweka wazi na anaendelea kuchukua hatua bila kumuonea mtu." -aliongezea Mzee Yusuph Makamba.