Yusuph Makamba na Kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yusuph Makamba na Kiingereza

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Easymutant, Aug 10, 2010.

 1. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mie toka nimeanza kumjua Yusuph Makamba sijawahi kumsikia akiongea hata neno moja la Kiingereza ila
  ni kwamba ni bingwa wa kukariri mistari ya biblia na ya kwenye misahafu..
  sasa kuna mtu ananibishia sana anasema jamaa yuko fiti kwenye hiyo lugha ya kiingereza ila hapendi kuitumia tu ... wanaomfahamu vyema mnisaidie maana inawezekana nikawa nabisha bila kufahamu.

  Asanteni.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nilimsikia akiwaomba wajumbe wa mkutano mkuu kura na kibwagizo "I Love you all" nadhani hiki ni kiinglish

  Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you

  June 11, 2007
  Na Beatrice Bandawe, Dodoma


  Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, (pichani kulia) juzi alilazimika kuwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kura kwa kutomhukumu kwa mabaya yake na kuwaambia: `Ilove you`.

  Bw. Makamba ambaye mara baada ya kuwaambia wajumbe hao `I love you` (nawapenda), waliripuka kwa mayowe ya vicheko, alisema kuwa binadamu yuko mara tatu.

  Alifafanua kwamba upande wa kwanza wa binadamu ni vile anavyojifahamu mwenyewe, anavyofahamika na wenzake na anavyofamika na Mungu.

  Alisema kwa jinsi anavyojifahamu yeye, anafaa kuchaguliwa katika uchaguzi huo.

  Bw. Makamba ambaye aligombea kundi la viti 20 la NEC Taifa, hata hivyo, alichaguliwa kwa ushindi mnono.

  `Chonde chonde wajumbe nichagueni I Love you,` alisema kwa kuweka msisitizo.

  Aliwataka wanachama hao kutomhukumu kwa mabaya yake kwani hata Mungu aliwasamehe waliomkosea.

  `Nawaombeni mninusuru na chama chetu,` alisema na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu aliochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, amepambana na kuwagaragaza wapinzani.

  Alisema kama wajumbe watamuangusha, hata wapinzani watafurahi na kusema CCM wameangusha Katibu Mkuu wao.

  Aidha, alisema vyombo vya habari pia vitapata ya kuandika na kuweka kwenye vichwa vya habari kwamba Makamba agaragazwa na wana-CCM wenzake.

  Bw. Makamba ambaye alikuwa akitoa kauli hiyo wakati aliposimama kwenye jukwaa la kuombea kura, mara baada ya kumaliza kujinadi, Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, alimjibu kwa kumwambia: `We love you too,` na kusababisha ukumbi mzima kushangilia.


  SOURCE: Nipashe


  Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Makamba kielimu yuko duni, nasikia tetesi kuwa aliwahi kuwa mwalimu wa UPE, ambako sijui alihusishwa na tukio la ubakaji mtoto wa shule, kisha akadondokea Jeshi , ni darasa la saba fulani hivi, ni sawa na kina Lukuvi, na Tz kama hujaenda shule nafasi yakuongea kingereza ni ndogo, maana hakizungumzwi mtaani.
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tutasikia mengi huku! Ila kiukweli hata mm sijamsikia mgosi akilonga kiinglishi hata siku moja. Tuambieni anakimanya ama
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimecheka sana leo.....kweli this is good observation! Ndio maana sijasikia Makamba katumwa kuhudhuria mkutano wa vyama rafiki mfano ANC etc
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sijawahi kuona mtoto wa Mfalme Malaria Sugu hata aandike neno moja la Kiingereza!
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mbowe anaongea English tangu nursery school, hahaaah Kilaza wewe bana. utamuona wapi wakati wewe unashinda pale kwa wauza kahawa SUWATA,
   
 8. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Haa haa haaa! Mwaka huu yataibuka mengi sana, na nyingine iko HAPA

  Mgombea CHADEMA ataka mdahalo na Makamba

  na Kulwa Karedia, Tarime

  MGOMBEA ubunge wa Tarime kwa tiketi ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Charles Mwera, ametaka uwepo mdahalo wa lugha ya Kiingereza kati yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwera, alisema amefikia hatua hiyo baada ya Makamba kutoa matamshi kwamba mgombea huyo hana uwezo wa kuzungumza Kingereza hivyo, hawezi kuwa mwakilishi mzuri wa wananchi bungeni.

  “Ndugu waandishi wa habari napenda kuwaambia kwamba mimi niko tayari kufanya mdahalo na Makamba, ili tuweze kuona nani anaweza kuzungumza vizuri lugha ya Kiingereza... kwani amekuwa akitoa maeneno ambayo si mazuri,” alisema Mwera.

  Alisema kitendo cha Makamba kumwambia hajasoma, kinaonyesha wazi jinsi Katibu Mkuu huyo wa CCM anavyotumia propaganda za uongo kutaka kuwahadaa wananchi wa Tarime kuacha kuichagua CHADEMA kwa madai kuwa itapata mbunge asiyejua lugha ya Kiingereza.

  Alisema kitendo cha Makamba kinaonyesha wazi kwamba yeye hana elimu ya kutosha, hivyo ananza kujihami kabla ya kutaka wakutane kupambanishwa kwenye mdahalo huo ambao ndio utakaotoa jibu sahihi.

  “Namwomba ndugu Makamba atambue kwamba mimi sijatoka kijijini bwana... naelewa lugha nyingi zikiwemo Kijerumani, Kifaransa, sasa yeye aje aniambie anaelewa lugha gani zaidi ya Kiswahili tu... dawa tukutane tu,” alisema Mwera.

  Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu madai hayo, Makamba alisema yuko tayari kukutana naye kwa ajili ya mhadahalo huo watu wajue kwamba yeye si ‘Maimuna’.

  “Mimi nasema kwamba niko tayari kupambana naye kama mwenyewe anavyotaka... sisi CCM tunatumia sera na kanuni za chama sambamba na ilani yetu... sioni kama kuna tatizo bwana… kilichopo nikutaka kushinda jimbo hili, nadhani umenielewa,” alisema Makamba.

  Vyama vya CCM na CHADEMA vimekuwa katika mvutano mkubwa katika kampeni zinazoendelea hivi sasa, huku kila kimoja kikionekana kuwa na mashabiki wengi, hali ambayo inasababisha uchaguzi huu kuwa mgumu na kushindwa kutabiri nani ataibuka mshindi.

  Uchaguzi huo utafanyika Oktoba 12 mwaka huu, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki dunia Julai 28, mjini Dodoma, kwa ajali ya gari.

   
 9. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi mmekosa cha kujadili?
   
 10. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwani kiingereza ni nini? Ukijua kuongea ndio unakwenda peponi au? Kiingereza sio lugha tu? Nasikia Wachina watakuwa wanaongoza kwa utajiri na kuwaacha mbali USA, Je wanaongea kiinglishi kuwazidi USA? Vipi Wajapan, Wajerumani? Ma-taliano ooPs Italy, je, Wagiriki, Portuguese, France, Sweeden, Norway, Russia etc the list goes on and on Oooops zipo nchi tele ambazo zinatumia lugha zao za asili wala hawababaiki na lugha ya wakoloni.

  Makamba kama anfahamu hii lugha au la haisaidii kitu, Huyu Makamba anatimiza wajibu wake kama kiongozi anayefaa? Hilo ndio swali la msingi!


  Pengine ukijua hii lugha unakuwa mkoloni zaidi kuliko wakoloni wenyewe - angalia Kenya.
   
 11. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  La muhimu ni kwamba anajua kuzungumza kiswahili, kwa hivyo anaweza kuwasiliana na asilimia kubwa sana ya watanzania. Na wale wasiofahamu basi wajifunze kisambaa.
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HAPA MJADALA UTAKUWA UMEVAMIWA......ni sawa na kusema MBOWE KAFELI MASOMO......au MBOWE ANAMILIKI CLUB BILLICANAS ambapo machangu,bangi,mashoga, unga na UCHAFU WA KILA NAMNA UNAPATIKANA ndiye mwenyekiti wa chama cha siasa....CHAMA HIKI KIKIPATA MADARAKA SI KITARUHUSU NDOA ZA MASHOGA?
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Hebu ngoja nianze ku dig information kuhusiana na hii kashfa.
  naomba Malaria Sugu atoe ufafanuzi
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Tunamjadili Makamba....hulazimishwi kushiriki lakini...unasamehewa kwa ugeni wako
   
 15. C

  Cool Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  No problem, makamba anaiweza siasa, mtaalamu wa propaganda. Lakini Watanzania wangapi wanaweza kuongea Kiingereza? Kwa nini iwe lazima kujua Kiingereza wakati Watu unaowaongoza wao huongea Kiswahili?
   
 16. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Yawezekana chakuombea maembe na machungwa rushoto anakijua lakini kwa background yake nikwamba kipindi yupo jeshini hapakuwepo wasomi hivyo yeye kuhitajika kujua au kutojua aikuwa issue kwake!!Nakipindi hicho ccm hadi majeshini yawezekana alikuwa kada ndiyo maana akaishia cheo cha luteni!!ila kwa misamiati yakiswahili na vibwaizo....utamtaka:smile-big:
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,632
  Trophy Points: 280
  Kumbe ushamtoa kwenye ile listi yako?
   
 18. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sisi tumsifu tu huyu mzee kwa uwezo wake mkubwa wa kuenzi Luga yetu ya taifa! Ila chama chake ndicho kilichopendekeza kiingereza kiwe official language!
   
 19. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kupenda kuongea kiingereza ni kuendekeza ukoloni mambo leo, nenda france au germany halafu kajifanye unapenda kuongea kiiingereza ndio utaona kitakacho kutokea,ni vizuri kupenda lugha yetu adimu ya kiswahili so Makamba hana kosa ila anadumisha lugha.Hivyo hivyo Mgosi ongea hata kishambaa tutakuelea kwani wote sisi ni wabantu, kama ni mbwai mbwai halafu ekai mambeza kabisa inywi.
   
 20. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Kwani ni mwingereza? Mimi huwa nadhani ni mwenyeji wa Tanga!
   
Loading...