Yusuf Manji kupambana na Antony Dialo jimbo la Ilemela 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yusuf Manji kupambana na Antony Dialo jimbo la Ilemela 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shomari, Nov 25, 2009.

 1. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kutokana na kuwepo kwenye kiti cha ubunge kupitia jimbo la Ilemela bila kuwepo na mafanikio ya kutosha, kuna tetesi kwamba wananchi wa jimbo hilo hawana mpango wowote wa kumpatia kura ndugu Dialo bali iwapo ndugu Yusuf Manji atagombea basi watampatia ushindi bila wasiwasi .
  Swali: kuna yeyote anayejua lolote kuhusu hili atumwangie humu ndani ?

  Pili; Mr Manji ni kweli una mpango huo? sababu wananchi wa Ilemela na Kayenze wanakuhitaji sana

  asante.
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani Manji amefanya nini kwa jamii yoyote ile hadi watu wamuhitaji sana?
   
 3. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .......Kama ni kweli basi siasa zetu zimefika kubaya.......Imefika wakati tuanze kuangalia mikakati ya nini wawakilishi wetu watatufanyia Jimboni badala ya kuangalia ukubwa wa hongo wanazotuma wakati wa uchaguzi...
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  we will be doing justive to ourselves iwapo tutapunguza tetesi hizi sizizo na vicwa wala miguu
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya akina Masatu yanazidi kushikakasi nchini tz hasa kumsifia mtu kwa sababu tu ana pesa bila kujali kaitendea nini jamii inayomzunguka.Wakazi wa Ilemela"wamuhitaji sana tajiri Manji kwa kipi hasa alichowafanyia"?Upupu kama huu mods muwe mnautoa jamani!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,570
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  I certainly do i agree with you,hata hivyo kwani Diallo si alichaguliwa kwasababu ya utajiri?Sijui ni yepi hayo aliyowafanyia wananchi huyo ndugu Diallo ila ana vyombo vya habari kama Redio Free Afrika nadhani na Star tv kama sikosei.
  BTW Manji ni mwenyeji wa Mwanza ama ni mikakati tu ya mafisadi?
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  wamesema siasa na biashara haitakiwa, sasa huyu manji si ni mfanyabiashara?
   
 8. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nogopa kuchangia maanake natokea morogoro ambako wananchi wake wanaamini kuwa ponjoro wanafaa kwa maendeleo ya jimbo....juzi juzi nikasikia kuwa kilombero hawamtaki aliyepo na wazee wa huko wapo katika mazungumzo na yule mwenye mabasi ya dar-moro achukue fomu ya ubunge....ni tetesi tu !
  Ila kama ni kweli inanipa picha ya mababu zetu kina kimweri,rumanyika na mirambo ukimuondoa mkwawa....jinsi gani hata na wao nao walifikiri kama sisi (ilemela,kilombero) tunavyofikiri.....tunarudi kule kule alikotutoa mwalimu, maana hata viongozi wetu wanafikiri hivi hivi kama sisi (ilemela,kilombero) tunavyofikiri...mie nakuambia baada ya miaka KADHAA hapa hapatatosha....maana sidhani kama hawa
  watoto wetu ambao hawajakimbia mchaka mchaka na kuimba chipukizi, na kujipanga barabarani siku nzima kumsubiri mtu anayepunga mkono,kusoma hadithi za brown ashika tama, kuimba fikiri mi maskini uvivu wangu nyumba wala hawajui kama kuna jogoo aliyesema baada ya kuteswa na pazi WATAKUBALI UENDAWAZIMU HUU


  A woman can be strong,confident and sexy

  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ujinga mtupu....
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama huna cha kuchangia heri unyamaze tu... unakuwa kama sio mjinga!
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,719
  Trophy Points: 280
  NI HUYU TAPELI WA JIJI HAPO CHINI EMBU NISAIDIEN KABLA YA KUANZA KUTOA MAONI

  Manji akumbwa na balaa
  • Manispaa Kinondoni kumfikisha mahakamani


  na Betty Kangonga
  HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Manji, kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.

  Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo, ambaye alibainisha kuwa, halmashauri hiyo ilimpatia zabuni ya kuagiza matela mfanyabiashara huyo, lakini ameshindwa kulinda makubaliano ya mkataba.

  Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Manji hana nia ya kupeleka matela yenye viwango vinavyohitajika au kurejesha kiasi cha shilingi milioni 324 alichopewa kwa ajili ya kazi hiyo.

  Bujugo alisema matela 27 yalikusudiwa kusambazwa katika kata zote za wilaya hiyo ili kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.

  Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.

  "Zabuni hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha miezi mitatu, lakini Manji alikiuka utaratibu huo ambapo imepita zaidi ya mwaka ndiyo anatuletea matela hayo yasiyo na ubora," alifafanua Bujugo.

  Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.

  "Sisi tuna ushahidi wa kile tulichokiagiza katika makubaliano yetu. Tulihitaji kuletewa matela yenye matairi manane, amechukua muda mrefu anatuletea matela ya matairi manne, hatuyataki," alieleza.

  Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.

  Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.

  Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.

  Alidai kwamba pamoja na agizo hilo, mfanyabiashara huyo alishindwa kutimiza masharti aliyopewa, jambo lilioifanya manispaa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha jambo hilo linamalizika.

  Tanzania Daima Jumatano lilijaribu kumtafuta Manji ili kuzungumzia sakata hilo, lakini simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake.

  Msaidizi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Manji hakuwepo ofisini huku akilitaka gazeti limuachie maagizo ili akirudi ampe.

  "Ninaomba uniachie ujumbe nitamfikishia na kama atakuwa tayari najua lazima atakupigia," alieleza msaidizi huyo.

  Hata hivyo, msaidizi huyo alishindwa kutimiza ahadi hiyo ambapo hadi Tanzania Daima Jumatano linakwenda mtamboni, hakuna simu yoyote iliyopigwa na Manji.
   
 12. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hii lugha nimeipenda, imekaa kidiplomasi sana
   
 13. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Manji?!!!
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Njaa mbayaaaa. Ila kama Manji atachukua form itakua ameonyesha dharau kubwa sana kwa watanzania kwani hafai na hakubaliki.
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,897
  Trophy Points: 280
  Nani kakupa hiyo nafasi ya kuwa msemaji wa watu wa Ilemela na Kayenze? Acha kuwaaibisha watu wa Ilemela kwa kuwaambia eti Manji awe mbunge wao. Kama wewe unamuhitaji kakae nae kwako.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  MAnji hataki tena Kigamboni??au mnampimia upepo Diallo
   
 17. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #17
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli! Nakubaliana na wanaosema njaa zinawasumbua watu, wanaona kwa Manji wanaweza kunufaika na hongo inayotokana na damu zao wenyewe -- maana wao ndiyo walioibiwa na kisha mwizi 'Manji' anakuja na "fadhila".

  Unaweza ukashangaa watu kwa sababu za kijinga tu wanachagua jambazi na kurudisha enzi za kabla ya mwalimu
   
 18. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Manji amekutuma??? au unamuomba kwa ujinga wa umaskini wako, kama angefaa ccm ingemuacha agombee kigamboni...............
   
Loading...