yUsuF MaNjI kUleTa kAmPuNi MpYA yA sImU Za mKoNoNi wIkI mBILi zIjAzO kUanZiA jAnA

********* huyo wahindi bahili sana hiyo kampuni haitafika kokote cheki sasatel na HITS zimeishia wapi kuna benson nayo mpaka leo haikuwi

Hili ndilo tatizo letu Watanzania, kutotakiana mema; lakini nakuhakikishia kama wangesema wawekezaji kutoka nje (wazungu) ndiyo wanaleta kampuni mpya ya simu za mkononi-basi wala kejeli hizi husingezisikia. Mimi nafikili tumpe pongezi za dhati Ndugu Manji kwa kujikita katika sekta hii muhimu ya mawasiliano; kijana huyu ana uwezo mkubwa wa kibihashara na ni mbunifu sana, nakwambia atawashangaza wengi.

Nimeona jamaa humu kazungumzia pia Sasatel na kampuni nyingine kwamba hasikuwi, nataka kumfahamisha kwamba Sasatel shughuli zake za msingi ni kusambaza mtandao wa Internet kwa wateja wakubwa na wadogo na wamefanikiwa sana katika hilo, siyo vizuri kubeza beza watu.
 
Kampuni mpya ya simu za mkononi ya MYCELL inayomilikiwa na mfanyabiashara wa kitanzania yusuf manji, inatarajia kuanza kutoa huduma zake katika kipindi cha siku 15 zijazo kuanzia jana.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake dsm juzi mkurung3nzi wa ufundi wa mycell kanali anurag chandra alisema kampuni hy ni dada wa kampuni ya quality group.
Mycel imezingatia ubora wa huduma kwa wa2miaji wa handmobile na inauwezo wa 3.5G
Ni kampuni ya kwanza ya handmobile kumilikiwa kwa 100% na mtz


Kampuni hyo itazingatia kuajili watz zaidi.
Source tz daima na irene mark.

Mkuu, huyu jamaa kachelewa watu wameshaota mizizi kwenye mitandao ya awali, kuhamahama kuna usumbufu. Hebu watazame zantel, kwa mtazamo wangu ni kwamba wana viwango vya chini kuliko mitandao yote lakini inafanyaje sokoni ukilinganisha na tigo,airtel na voda zilizotangulia? suala la msingi hapa ni timing, hata aje na viwango vya chini namna gani hawezi kuwabeat hao waliotangulia labda cc wa moderm tunaisubiri hiyo MYCELL kama itakuwa na speed nzuri na viwango vya chini tutaichangamkia fasta lakini siyo kwa wateja wa simu, its too late mate!
 
Mkuu, huyu jamaa kachelewa watu wameshaota mizizi kwenye mitandao ya awali, kuhamahama kuna usumbufu. Hebu watazame zantel, kwa mtazamo wangu ni kwamba wana viwango vya chini kuliko mitandao yote lakini inafanyaje sokoni ukilinganisha na tigo,airtel na voda zilizotangulia? suala la msingi hapa ni timing, hata aje na viwango vya chini namna gani hawezi kuwabeat hao waliotangulia labda cc wa moderm tunaisubiri hiyo MYCELL kama itakuwa na speed nzuri na viwango vya chini tutaichangamkia fasta lakini siyo kwa wateja wa simu, its too late mate!

Naomba nitofautiane na wewe. Kuchelewa kuingia siyo kitu. Ila ni jinsi unavyojipanga. Kama kuwahi ndo hoja basi tritel leo ndo ingekua leading mobile services provider. Akicheza karata vizuri, the opportunity is still there.
 
hivi zimebaki siku ngapi vile ufunguliwe huo mtandao??
 
Karibu sana kwenye soko letu la ushindani mkubwa na utanue wigo wa ajira kwa watanzania!!!!!kazi ipo lakini maana ushindani ni mkali sana!
 
Kiukweli, inabidi apongezwe. Anastahili. Imagine kampuni ya simu kumilikiwa 100% na mtanzania! Vodacom nadhani 60% ni UK. Airtel 100% India(Jina kamili Bharti Airtel), Zantel ni wa TZ (Sina uhakika sana kama ni 100% wa TZ). Tigo nadhani asili yake El Salvador makao makuu Luxembourg. Wasi wasi wangu ni kwamba, Manji anaweza akawa anatumiwa kama njia tu kuingilia na ana 25% za kampuni yote. Kila la kheri.
 
Mimi naomba tuu waniletee internet bomba zaidi ya airtel na nafuu pia mie nitahamia huko bila kufikiria mara mbili. Huu ndo ushindani tunaotaka karibu sana na usisahau zile promotion za bure kama za tigo basi wengi siye tutakuja kwako
 
Hizo kampuni zote ulizozitaja hapo juu zimeangushwa na mfumo wa teknolojia wanayotumia ya CDMA ambayo ni ya kisasa na ni gharama kubwa kuweza kuiendesha ndio maana BENSON Online wamekufa kimya kimya wakifuatiwa na wenzao SASATEL


Kama kampuni ya Mycell itakuja na mfumo wa GSM ambao ndio umesambaa zaidi hapa nchini itakuwa ni rahisi kwake kwenye upande wa uwekezaji hasa kwenye upande wa celltower ambapo anaweza kutumia minara ya makampuni yaliopo badala ya kujenga ya kwake kitu ambacho TCRA hataki kutokana na uharibifu mkubwa wa maziringa hivyo sheria ya sasa inawalazimisha kushare mirana..


Kwa upande wa soko inategemea na plan zake za kuweza kuliteka soko kwa kuja na huduma za uhakika na bei nzuri,na kujua ni nini hasa wateja wanahitaji

Nani kakwambia hawawezi share tower ?kwa nini waziweze share?

Sema kushare antenna! ila tower wanashare kama kawa ...basi kwa taarifa yako running cost ni ndogo kwa 4g &3g 3.5g compare to 2g 2.5g but intial cost ndio kubwa .
 
Hiyo kampuni mbona kimya tena ama ndo wamefulia hata kabla ya kuizindua?
 
dah mie nilidhani kuna mpya yoyote. kumbe nawe unakumbushi......
 
Back
Top Bottom