Yusuf Manji kuhamishia biashara zake zote nchini Zambia

Alafu anatokea MTanzania na elimu yake ya chuo, bila hata kujituma kufikiria anaanza kusema waTanzania watakosa ajira akiondoka Manji... What the hell is he benefiting from Manji ??
Watakao kosa ajira ni wahindi wenzake sababu hawa watu hawaajiri watanzania kwenye zile sehemu zenye maslahi hata akikuajiri hatakupa mshahara ambao atampa muhindi Mwenzake nashangaa sana wabongo wanawaowaona hawa watu ni wa maana kumbe ni watu wa hovyo tu

Yupo radhi amtoe muhindi Mwenzake India aje amgaramikie gharama zote mpaka Tanzania na gharama nyingine za maisha awapo kwenye company yake kuliko kumpa hiyo ajira mtanzania na kumlipa mshahara mzuri. Alafu wanajiita watanzania, kiswahili tu chenyewe haongei sijui mtanzania wa wapi.
 
Tajiri kukubali kuishi kama shetani ni matumizi mabaya ya akili,wengi walihamishia Pesa zao Kenya, south Africa biashara walizihamishia Zambia,Congo,Malawi,Msumbiji,hata malori mengi yamehamishiwa huko yanakwenda maputo yanachukua mizigo kupitia Malawi wanaendelea kutengeneza Pesa kama kawaida,masikini hana uwezo wa kumkomoa tajiri.Sisi ndio looser mfano watu zaidi ya laki moja wamekosa Kazi hawa ni sh ngani walichangia mifuko ya jamii kila mwezi si chini ya sh laki moja kila mwezi, ujaja kodi, mamlaka zote kuanzia OSHA, Sumatra, TBS, tfda,TRA, halmashauri, nk ni kiasi gani mapato yao yameathirika yamepungua kwa watu kuhamisha mitaji nje.Kiuchumi kanuni ya namba iko hivi ukisomesha watu namba wakimaliza kuisoma namba lzm mgawa namba uisome pia inaitwa cause and effect principal, maana mashetani sasa hayana uwezo wa kuchangia mifuko ya jamii,tajiri wa kuchangia mifuko ya jamii na kodi na Tozo zote either kafilisika au kahamisha nje mtaji wake,matokeo yake ni kukauka kwa kibubu sawa na kuizuia mifereji iingizao maji bwawani.Kibubu kikikauka utashindwa kuhudumia watu ukishindwa kuhudumia watakuchukia,chuki na hasira zikizidi watatafuta mabadiliko popote pale kujinasua na hali.

Jiulize maswali madogo tu:

1) Viwanda vilivyobinafsishwa viliongeza pato gani kwa Taifa? Tumeshuhudia kwa wafanyakazi kupoteza ajira. Wewe unadai Sisi ndio looser mfano watu zaidi ya laki moja wamekosa Kazi

2) Hao matajiri wameisaidia nini nchi hii? Tumeshuhudia mwongezeko wa machinga, na vitu visivyoongeza pato la Taifa, km mahoteli na supermarkets yakiuza bidhaa za nje hata nyanya na nyama ya kuku. Wewe unadai Kibubu kikikauka utashindwa kuhudumia watu ukishindwa kuhudumia

KUPANGA NI KUCHAGUA
 
Kuna wakati huyu manji alikuwa anatukanwa sn kuwa ni fisadi mkubwa.ni moja kati ya waesha wanaoifirisi nchi.au mm naota mchana??
 
Manji alikuwa anatuona Watanzania wajinga sana, katuibia sana Watanzania wacha ayumbishwe tu akili zimkae sawa. Ule ujinga wa kununua viwanja kigamboni kwa Mil 4 na kuja wauzia NSSF Bil 1.2 hata upata sehemu nyingine yeyote Duniani
 
Watakao kosa ajira ni wahindi wenzake sababu hawa watu hawaajiri watanzania kwenye zile sehemu zenye maslahi hata akikuajiri hatakupa mshahara ambao atampa muhindi Mwenzake nashangaa sana wabongo wanawaowaona hawa watu ni wa maana kumbe ni watu wa hovyo tu

Yupo radhi amtoe muhindi Mwenzake India aje amgaramikie gharama zote mpaka Tanzania na gharama nyingine za maisha awapo kwenye company yake kuliko kumpa hiyo ajira mtanzania na kumlipa mshahara mzuri. Alafu wanajiita watanzania, kiswahili tu chenyewe haongei sijui mtanzania wa wapi.

Ni kweli kabisa Mkuu (Your so Analytical Brother)..... Wahindi hawaajiri waTanzania hata siku moja, lakini akili ndogo wanapenda kuwasujudia.
 
Siku na ww ukianza biashara ndi utajua umuhimu wa makando kando,kodi zenyeww ndo hizo zinaenda kununua madiwan.
Kwenye biashara mimi ni mdau, tena mwenye uzoefu mwingi. Ni kweli ndugu yangu huku ni lazima kuwe na michongo la sivyo hupati kitu. Lakini suala la huyu jamaa ni ile inayoitwa tamaa ya fisi ambayo mimi ndiyo huwa nailaani. Upigaji wa sampuli yake siutaki na bora nibaki na kidogo nilicho nacho
 
Watakapokosa hela za kulipa mishahara ya watumishi na za kulipa madeni,hasa ya nje,ndio watajua uongozi ni busara na si mabavu.
Tutakosaje kulipa mishahara?utasubiri sana
Hatutaki biashara za ujanja ujanja waondoke tu
 
Kwa taarofa yako hiyo kampuni inadaiwa na mabenki na pesa haramu iliyokuwa inatumika kuiendesha haipatikani tena.
Wewe hujui wafanya biashara na masuala ya kuhamisha mitaji(release of capital)

Kama akili yako inakuaminisha hivyo, basi huko Zambia Manji anaenda kucheza gombesugu.
 
Wanajamvi kumekuwa na tetesi za chini chini kuwa baada ya kuandamwa na serikali ya awamu ya tano kwa muda mrefu mfanyabiashara Yusufu Manji kuhamia Zambia. Habari kutoka kwa watu wa karibu zaidi na familia ya mfanyabiashara huyo zinasema mpaka sasa makampuni yake matatu yameshafungwa bado yupo katika hatua za mwisho wa kufunga biashara zilizobaki
View attachment 957252
Na uelezee manji kupitia quality group of companies alivyojipatia mabilioni kitapeli kwa kutumia raslimali za NSSF,
Usiishie kutueleza pia alivyojitangaza muflisi kitapeli ili aweze kukwepa madeni...vyuma vimekaza
 
je ?mmepata mbadala wa shughuli alizokuwa anafanya?
Jiulize maswali madogo tu:

1) Viwanda vilivyobinafsishwa viliongeza pato gani kwa Taifa? Tumeshuhudia kwa wafanyakazi kupoteza ajira. Wewe unadai Sisi ndio looser mfano watu zaidi ya laki moja wamekosa Kazi

2) Hao matajiri wameisaidia nini nchi hii? Tumeshuhudia mwongezeko wa machinga, na vitu visivyoongeza pato la Taifa, km mahoteli na supermarkets yakiuza bidhaa za nje hata nyanya na nyama ya kuku. Wewe unadai Kibubu kikikauka utashindwa kuhudumia watu ukishindwa kuhudumia

KUPANGA NI KUCHAGUA
 
Uadui na mkuu alijenga yeye mwenyewe.
UKiwa na fedha punguza jeuri na kibri be humble maisha yataenda.
Ingawa wapo wanaosema mpaka kufika apo kwa kiasi kikubwa ni deals za mjini sasa kama zimebanwa lazima uamishe kijiwe.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom