Yusuf Manji kuhamishia biashara zake zote nchini Zambia

Sio Manji pekee Wafanyabiashara wengi wamekimbilia Zambia,Uzuri wa Zambia ukiwalipa kodi hawakusumbui tena na hawana EFD wala ujinga wa risiti na ndio Nchi ambayo mizigo mingi inaingia kutoka SA na China kupitia Durban maana Tanzania walikimbia baada ya kuwekewa VAT kwenye transit goods sasa imefutwa wao washazoea tena SA...bandari zipo nyingi mnaleta usumbufu watu wanaangalia kwenye unafuu tu..
Vipi usipolipa kodi au ukilipa kodi chni stahiki yako!
 
Hii nchi kwa sasa wakwepa kodi watakimbia..ila zambia huko nako si atalipa kodi tu au nako ataachwa?
Kule kodi ni rafiki sio za kukomoana kwanza maafisa wa zra mwenyewe utapenda ukisema sina wanasema Jitahidi wanaondoka zao hata wakija siku nyingine ukiwapiga saundi hawana neno ila wewe mwenyewe dhamira yako itakusuta sababu kodi yenyewe ni ndogo.

Sasa huko Tanzania kwetu ukisema sina tayari washafunga mlango sasa nitazikuta wapi pesa za kuwalipa mnapofunga mlango? Mbuzi nyie wanatia hasira sana.
 
wananchi katoeni fedha zenu kwenye mabenki ya ndani mtakuja kulia kilio cha paka shume....na tuache kuspend hela kwa vitu unnecessary....Isaya 55:2 Kwa nini mnaendelea kulipa pesa kwa ajili ya kitu ambacho si mkate, na kwa nini kazi yenu ni kwa ajili ya kitu ambacho hakishibishi?....Baada ya miezi sita Jiwe ataomba kung'atuka...
 
Sidhani kama Manji anaweza kufanya biashara halali bila makandokando. Kama ameamua kuondoka kweli basi ni nafuu kubwa kwetu Tanzania.
Siku na ww ukianza biashara ndi utajua umuhimu wa makando kando,kodi zenyeww ndo hizo zinaenda kununua madiwan.
 
True
Sio Manji pekee Wafanyabiashara wengi wamekimbilia Zambia,Uzuri wa Zambia ukiwalipa kodi hawakusumbui tena na hawana EFD wala ujinga wa risiti na ndio Nchi ambayo mizigo mingi inaingia kutoka SA na China kupitia Durban maana Tanzania walikimbia baada ya kuwekewa VAT kwenye transit goods sasa imefutwa wao washazoea tena SA...bandari zipo nyingi mnaleta usumbufu watu wanaangalia kwenye unafuu tu..
 
Tangu nizaliwe,kwa mara ya kwanza ,nashindwa;
1.Kulipa kodi ya nyumba
2.Kulipa mishahara ya h/girl na h/boy
3.Kununua mafuta ya gari
4.Kulipa ada za shule za watoto
5.Kununua Luku
6.Madeni kibao

Nimemuomba Mungu sana nisifikie hapa, naona maombi yamebuma...labda ndiyo maana ya kuishi kama shetani
 
Sio stationery tu hata Madawa ya binadamu serikali ilikua inatoa tender ya suppliers utafikiri viwanda vipo Mars kwa serikali haiwezi kununua dawa moja kwa moja kiwandani mpaka imtafute dalali wa katikati, huo wote ulikua ni ufisadi mwisho wa siku dawa inayouzwa 500 kiwandani serikali inanunua kwa 1300 sababu ya muhindi na viongozi fisadi wamekaa hapo kati lakini saivi jamaa kakata huo mrija MSD yenyewe inaenda kununua moja kwa moja viwandani sasa wale waliokua na tender saivi wanalimia meno

Hali kadhalika na haya mashangingi ya serikali kuna company ilikua inadalalalia yaani kana kwamba serikali haijui Japan ipo sehemu gani iende ikanunue magari yake yenyewe eti mpaka dalali aingie kati, saivi zile showrooms za Toyota Tanzania ambao ndio walikua walanguzi wa magari yote ya serikali wanauza bajaji na pikipiki za toyo kwenye showrooms zao maV8 yameota mbawa,
Huyu Manji nae ni ukosefu wa tenders za kipuuzi za serikalini kama hizi ndio zilikua zinamfanya Don kuanzia tanesco mpaka jeshini jamaa alikua ana tender balaa, saivi hapati hata tender ya sindano serikalini.


Kweli huyu jamaa ni shida


Alafu anatokea MTanzania na elimu yake ya chuo, bila hata kujituma kufikiria anaanza kusema waTanzania watakosa ajira akiondoka Manji... What the hell is he benefiting from Manji ??
 
Tangu nizaliwe,kwa mara ya kwanza ,nashindwa;
1.Kulipa kodi ya nyumba
2.Kulipa mishahara ya h/girl na h/boy
3.Kununua mafuta ya gari
4.Kulipa ada za shule za watoto
5.Kununua Luku
6.Madeni kibao

Nimemuomba Mungu sana nisifikie hapa, naona maombi yamebuma...labda ndiyo maana ya kuishi kama shetani

Kwani Burazaaa.... Mshahara wako umepunguzwa au umefukuzwa kazi ? au ulikuwa kwenye list ya wapiga dili na mishahara hewa ??
 
Hivi waweza rudia kusoma hiki ulichokiandik na kuridhika kabisa kuwa uwezo wako ndiyo huu? Je nkikuita ni mpumbavu ntakuwa nimekutusi au kukuonea? Anyway busara si kwa wote

Darja zaidi ya mpumbavu ni lipi? Nisaidie ili nikuambie kwa nini huwezi kunielewa.
 
Tuna rais wa ajabu haijawahi tokea.

Ni kweli kwa sababu... ndio Rais wa kwanza kutujengea Reli ya Kisasa, wengine hata ya kizamani walishindwa, ndio Rais wa kwanza kutuletea Bombardier 3, Dreamliner na Airbus ya kisasa kabisa wakati wengine walichemka kuendeleza hata zilizokuwepo, ni Rais ambaye anatuletea Umeme wa bei rahisi wa Stiglers Gorge wakati wengine walizidiwa akili na Habinder Singh, ni Rais ambaye ametetea wakulima walipwe bei nzuri ya korosho wakati wengine walishindwa, ni Rais anayetujengea Flyovers Tanzania wakati wengine walishindwa, ni Rais aliyehakikisha wanafunzi wanalipwa Boom zao kwa wakati wakati wengine walishindwa, ni Rais aliyedhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali wakati wengine walishindwa, ni Rais aliyeweza kujenga Daraja refu la Kilombelo pale ambapo kila mwaka waTanzania walikufa, ni Rais aliyejenga Mabarabara ya lami kuunganisha mikoa wengine walishindwa, ni Rais aliyejenga Hostel za UDSM na kuondoa adha ya kupanga mitaani, ni Rais ambaye amevunja rekodi ya kujenga vituo vya Afya takribani 67 na Hospitali kubwa za mikoa 18 wakati ilikuwa historia, ni Rais ambaye watoto wa wananchi wanaenda shule bure, yako mengi sana ambayo kayafanya kwa kipindi cha miaka mitatu tu, hatuwezi kuyaandika hapa yanayofanya umuone ni waajabu kabisa.

Na hasa unakuta kulakulala wengi wanafikiria ni bora hizo pesa zilizo tumika kufanya hayo mambo wangepewa wakajirushe Tripple 7 au Akira o_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_Oo_O.
 
Wache wajiindokee tu maana nchi hii sasa haitabiriki.

Watakapokosa hela za kulipa mishahara ya watumishi na za kulipa madeni,hasa ya nje,ndio watajua uongozi ni busara na si mabavu.
Unaombea mabaya nchi yako na siyo huyo unayemlenga ila ni dua potofu.

Kama wewe na MABWANA zako mna dhamira safi na nchi yenu, mjipange kwa Sera na Mikakati mbadala, zinazotekelezeka, za kuiendeleza nchi hii kijamii, kisisiasa, kiuchumi na kiteknolojia.

Lakini kwa jinsi mlivyojipambanua, nyie humu JF, mitandao ya kijamii, na viongozi wenu kwenye vyombo vya habari ni MAVUVUZELA tu kunadi hadithi za kusadikika.

Kwa yale yaliyofanyika na Serikali ya Awamu ya Tano, katika muda mfupi wa utawala wake, katika nyanja zote za maendeleo ya nchi hii, ni maradufu kuliko miaka yote kabla na baada ya uhuru.

ADA YA MWUNGWANA NI VITENDO na MANENO MATUPU HAYALAMBWI.
 
Back
Top Bottom