Yusuf Manji amtaka Mengi kuacha kumsakama na kumchafua kwenye vyombo vyake vya habari

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Mwenyekiti wa club ya Yanga bwana Yusuf Manji amemtaka Mengi kuacha kumsakama na badala yake aendelee na shughuli zake, Manji anamtaka bwana Mengi kuacha kutumia vyombo vyake vya habari vya IPP kumsakama kwani yeye anamuheshimu kama babu yake.

Katika kipindi hicho kinachoendelea kurushwa live na TBC muda huu ambao Mengi alialikwa ili authibitishie umma ufisadi wa Manji lakini hakutokea, hata hivyo Manji amesema kuwa yupo tayari kipindi kama hicho kiandaliwe tena na Mengi aalikwe tena ili aje kuthibitisha madai yake.

Manji amesema kuwa ni kwa miaka kumi sasa amekuwa akindikwa vibaya na magazeti na vyombo vya habari vya IPP vya bwana Mengi, alifika mbali zaidi kuvishangaa vyombo vingine vya habari pamoja na kuwa mara nyingi amekuwa akiita vyombo vya habari kujibu shutuma hizo lakini anashangaa asubuhi hakuna hata chombo kimoja kinachoandika.

Manji pia ametangaza kugombea udiwani kata ya Mbagara Kuu.

Chanzo: TBC
 
ha ha ha kaenda kutafuta umaarufu tu....eti anagombea udiwani ili apige zaidi hela ha ha bongo bwana...
 
Umaarufu gani anaoutafuta?hivi manji sio maarufu! Inawezekana operation kimbunga haikufanya kazi ipasavyo kuna wageni wengi tu
 
Ataingizaje ugomvi binafsi kuwa wa yanga kwani magazeti yaliandika chochote juu ya yanga
 
Ajabu mengi aliahidi kwenda tbc kuthibitisha madai yake halafu kaingia mitini, sijui tumuone ni mvushi au mgombanishi sijui anataka tumfikiriaje huyu babu.
 
Hivi kwenye udiwani kuna hela ya kupiga Manji? Ulishagombea ubunge Kigamboni alishinda kwa mbali kura za maoni wakamkata.

Mengi katoka nduki.

Teh teh teh
Maalim vipi! Ile ID nyingine unayotumia kiswahili fasaha hujaja nayo siku nyingi..
 
Mengi ni mvurugaji na ana tabia ya umimi sana, kwanini anapenda monopoly wakati biashara ya leo watu wanashindana? kwanini anawaona washindani wake maadui ama ndo hajaelewa kwamba soko ndo linanunua bidhaa na si shutuma za hovyo
 
Mengi ni ugomvi tuu kila kukicha,wakati wenzake wanapiga pesa kwa kwenda mbele.Mengi kawa mswahili kwa majungu
 
Ajabu mengi aliahidi kwenda tbc kuthibitisha madai yake halafu kaingia mitini, sijui tumuone ni mvushi au mgombanishi sijui anataka tumfikiriaje huyu babu.

atajifanya kuweka kipindi maalum ITV
 
Back
Top Bottom