Yusuf Manji amshitaki Reginald Mengi, adai fidia Sh1/-

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Manji leo amefungua kesi mahakama ya kisutu akidai amekashifiwa na Mengi. Anamtaka Mengi amlipe fidia ya sh1 kwa kumkashifu na kuandaa kipindu maalum cha kumuomba radhi ambacho atakuwa akikirusha (Mengi) mfululizo kwa siku saba
 
Du makubwa inamaana uharibifu aliofanyia pamoja na heshima yake kwenye jamii plus reputation ya makampuni anayoyaongoza gharama yake ni shilingi moja. Sikutegemea kama anaweza kuwa hana thamani kiasi hicho sasa naamini kuwa ufisadi unamshusha mtu thamani ya utu wake.
 
Manji leo amefungua kesi mahakama ya kisutu akidai amekashifiwa na Mengi. Anamtaka Mengi amlipe fidia ya sh1 kwa kumkashifu na kuandaa kipindu maalum cha kumuomba radi ambacho atakuwa akikirusha (mengi) mfululizo kwa siku saba


Mkuu MN, kama hutanii basi fanya marekebisho. Imekaa kama vile imetolewa kwenye "fools' day".
 
Mkuu MN, kama hutanii basi fanya marekebisho. Imekaa kama vile imetolewa kwenye "fools' day".
Ni serious Mkuu. Anadai Sh 1/-. nadhani lengo lake ni kutaka kumuonyesha Mengi kuwa tatizo lake si fedha
 
Ni serious Mkuu. Anadai Sh 1/-. nadhani lengo lake ni kutaka kumuonyesha Mengi kuwa tatizo lake si fedha

Au anataka kuufahimisha umma kuwa thamani yake kwa mujibu wake ni shilingi moja [kwangu hii inauzito zaidi kwa hilo lakuwa na fedha kwani hana sababu ya kulithibitisha kwani hata Mengi mwenyewe alikiri kuwa yeye (Manji) na wenzake wachache wanashikilia uchumi wa nchi hii, so hana sababu ya kurudia kuthibitisha hilo.]
 
Habari zaidi ni kuwa Rostm naye amemwelekeza wakili wake ampelekee Mengi demand note, akimtaka amuombe radhi la sivyo atamburuza mahakamani (natafuta details zaidi za hii)
 
Ni serious Mkuu. Anadai Sh 1/-. nadhani lengo lake ni kutaka kumuonyesha Mengi kuwa tatizo lake si fedha


May be na kuonesha pia kwamba yeye Manji ni PAPA tena LIPAPA. Lakini pia ni mjinga, au kama anavyoamini Watanzania ni Mabwege!!
 
Kiwango cha fidia kuwa kidogo hivi huwa inatokea, kuna wakati Paul Kagame, aliwahi kutaka fidia ya 1 franc kutoka kwa Rais wa France kwa madai ya kukashifiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki.

Pengine wanasheria watatuambia hii mana yake huwa ni nini?
 
Mengi's lawyers must have foretold this course of action & it's likely he has evidence he could use against the libel claim... or he could be an idiot...lol... but i doubt that.. ngojeni tuone.
 
Yaani hata mie nimeshangaa ila nilisikia tetesi kuwa Mzee Mengi hapo ndipo alipokuwa anapataka; pa kupelekwa mahakamani. Kama ni kweli basi tutegemee kusikia mengi katika hili.
 
jamani mlisikiliza kauli ya mengi ? Mengi hakumshutumu mtu, mengi aliwataja watu wanaoshutumiwa?????? hata hapa JF watu hao wanashutumiwa mtakubali kuwa mashahidi kuwa mnawashutumu watu hao?
 
Bw Manji Umefanya jambo Jema .... Usiwasikilize kina Mkuchika, Sofia Na Lipumba wao!!!

Mengi ..... Tulia vuta Subira. Angalia Mchezo kwa karibu na kwa mbali. Usome vema kabla Ya kuachia nondo!!

Al the best Sir!!!
 
Back
Top Bottom