Yusuf Manji akamatwa kutokana na malimbikizo ya kodi Tsh 300 milioni, ofisi zake zafungwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Temeke leo Oktoba 27 wamemkamata mfanyabiashara Yusuf Manji kutokana na kutolipa malimbikizo ya kodi anayodaiwa zaidi ya Tsh 300 milioni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastica Kivera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kwamba mbali na kumkamata Manji, pia wamefunga nyumba ya kuhifadhia mali (godown) pamoja na Ofisi yake iliyopo kando ya barabara ya Nyerere ili alipe kodi anayodaiwa na Serikali.

Yono ambao ni wakala wa ukusanyaji wa madeni ya Serikali kupitia TRA, wamesema kwamba wanamshauri Manji alipe deni analodaiwa ili waweze kufungua majengo yake wanayoyashikilia kwani kinyume na hapo watapiga mnada mali zilizopo ndani ya majengo kwa idhini ya TRA ili waweze kufidia deni hilo.

Kivera ameeleza kwamba, hatua ya wao kushikilia mali hizo ni kumtaka Manji alipe deni analodaiwa.
 
Back
Top Bottom